April 14, 2021

 


NAHODHA wa Yanga, Lamine Moro amefunguka kuwa, wanaodhani Yanga hawatachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, hawapo sahihi kwani akili za nyota wote wa kikosi hicho ni kuivua ubingwa Simba.

Kauli hiyo ni kama kuwachokonoa kimtindo mabingwa watetezi wa ligi Simba ambao nao hesabu zao ni kusepa na taji hilo.

 Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yaga ipo namba moja ikiwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 24 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 46 baada ya kucheza mechi 20.


Namba mbili ni Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ikiwa na pointi 47 baada ya kucheza jumla ya mechi 25.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Lamine alisema: “Wanaodhani kuwa sisi tumekata tamaa na ubingwa, wanakosea sana kwa sababu wachezaji wote hapa mawazo yapo kwenye ubingwa.

 

“Nimekuwa nikiona huko mitandaoni watu wakizungumza vibaya kuhusu timu na wanafikiri sisi tumekata tamaa, niwaambie kwenye maisha hakuna kukata tamaa, tutapambana hadi mwisho kuwania ubingwa wa msimu,” alisema Lamine na kuongeza.

 

 

“Tangu nimefika Tanzania sijawahi kuona mechi rahisi hasa kwa Yanga, ushindani huo umekuwa ukitufanya nasi tuzidi kuongeza juhudi ili kufikia malengo," .

6 COMMENTS:

  1. Masikini roho žao. Inaonesha watatumia nguvu na kufikia Mpaka Fifa kushtaki wanarogwa na kupigwa ushindi kwahivo wapewe ushindi wao wanastahiki

    ReplyDelete
  2. Mimi nawashauri Utopolo waelekeze nguvu zao zote kwenye kuiandaa timu yao kwa ajili ya kushiriki ligi ya mabingwa Africa ambako tayari wamekwisha kubebwa na Mnyama

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuingiza timu nne sio lazima Utopolo waende, wakikosa nafasi tatu za juu hawaendi

      Delete
    2. Mikia aka nyau mweusi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic