KOCHA Msaidizi wa Klabu ya Mtibwa Sugar, Soud Slim amesema kuwa wanatambua uimara wa safu ya ushambuliaji ya Simba inayoongozwa na Meddie Kagere na John Bocco wenye mabao tisa kwa kila mmoja.
Ikiwa ipo nafasi ya 15 na pointi zao ni 24 itapambana na Simba iliyo nafasi ya tatu na pointi 46.
Safu ya ushambuliaji ya Mtibwa Sugar imefunga jumla ya mabao 9 inakutana na ile safu ya ushambuliaji ya Simba ambayo imefunga jumla ya mabao 46.
Akizungumza na Saleh Jembe, Slim amesema kuwa:"Tunatambua kwamba wametoka kushiriki mashindano ya kimataifa na wana safu nzuri ya ushambuliaji, hilo tutalifanyia kazi kwa kuwa tunahitaji pointi tatu.
"Wachezaji wapo tayari na wanatambua kwamba kazi kubwa itakuwa baada ya dakika 90. Mashabiki wajitokeze sisi tupo tayari," amesema.
Mtibwa Sugar imetoka kupoteza mchezo wake wa ligi kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC inakutana na Simba ambayo imetoka kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi.
0 COMMENTS:
Post a Comment