UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweomba mashabiki na wanachama wa Yanga kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi pale wanapobaini kuna tatizo.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa tabia ya mashabiki kusema matatizo yao mitandaoni kila kitu hayaleti picha nzuri.
Baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC mashabiki wa Yanga walikuwa wakilalamika kwa kusema kuwa mwendo ambao wanakwenda nao hauwapi fuaraha zaidi ya stress.
Bumbuli amesema:-"Wanachama na mashabiki waache tabia ya kutaka umaarufu kwa kuzungumza, kama wameona tatizo baada ya mechi waje klabuni kusema au watupigie simu maana wanazo namba zetu.
" Ukisema unawapa faida vyombo vya habari halafu wachezaji wanawachanganya safari ya ubingwa inahitaji uvumilivu,".
Kwenye msimamo wa ligi Yanga ina pointi 51 ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 24.
Tutawapigia sana wao ndio wanacheza hovyo kabisa kama hawajala tutawapigia
ReplyDeleteTunawaambia wajirekebishe mpira unachezwa hadharan tunaona madudu yote yanayofanyika
ReplyDeleteSimu zenu zinakuwa zimezimwa au ziko bize, heri niongee tu na chombo cha habari nitoe ya moyoni nikalale kwa unafuu kidogo
ReplyDeleteTupige simu za nini na nyie hamtaki kubadilika. Hadi leo timu haina kocha wa maana. Mmekalia ubahili na hiyo gsm yenu. Angalieni wenzetu simba. Kocha safi uongozi safi ueekezaji safi mfumo safiii
ReplyDeleteWanazingua sana wachezaji. Mashabiki tunakosa AMANI kabisa
ReplyDeleteUwekezaji uko vizuri, shida ufundishaji mbovu mtu hajui hata mazoezi ya kuwongezea uwepesi wachezaji? Pili kamati ya ushindi sijui ipo au la, na kama ipo imelala usingizi.
ReplyDeleteKwani wakiongea kwenye media ujumbe haufiki? Au kwani wao wanapofanya utopolo wao uwanjani huwa wanatupigia simu kuwa wanaenda kufanya utopolo
ReplyDeleteDah inauma sana
ReplyDeleteNi kweli maneno ya mashabiki yanawachanganya wachezaji
ReplyDelete