April 18, 2021


 JOHN Bocco nahodha wa Simba ameonyesha umwamba wake leo mbele ya Mwadui kwa kufunga bao pekee la ushindi lililoipa pointi tatu mbele ya Mwadui FC ambayo leo Uwanja wa Kambarage ilicheza kwa nidhamu na kujiamini.

Dakika 45 Mwadui waliweza kuzuia mashambulizi ya Simba ambao walikuwa wakimtumia kiungo Rarry Bwalya na Clatous Chama kumtengenezea pasi Meddie Kagere na kufanya waende mapumziko ubao ukiwa Mwadui 0-0 Simba.

Dakika ya 66, Bocco alibaldili ubao ambapo ulisoma Mwadui 0-1 Simba na bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 90 na kuwafanya Simba kusepa na pointi tatu kwa tabu mbele ya wapinzani wake leo.

Kwenye mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, Simba ilishinda mabao 5-0 hivyo jumla wamesepa na pointi sita zote za Mwadui msimu huu wa 2020/21.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 52 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 212 imetofautiana pointi mbili na vinara Yanga wenye pointi 54 baada ya kucheza mechi 25.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic