VIVIER Bahati, kocha msaidizi wa Azam FC amesema kuwa bado hawajakata tamaa kwenye mbio za kusaka ubingwa kwa kuwa nafasi bado ipo.
Azam FC ipo ndani ya tatu bora na ilianza kwa kasi msimu huu wa 2020/21 jambo lililowafanya waje na sera yao kwamba wana jambo lao.
Kwa sasa ipo mkoani Dodoma ikiwa inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji, unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu ina pointi 50 baada ya kucheza mechi 26, nafasi ya pili ni Simba wenye pointi 52 baada ya kucheza mechi 22 na Yanga ni namba moja na pointi zao 54 baada ya kucheza mechi 25.
Bahati amesema:"Bado tuna mechi mkononi na kila mmoja kwa sasa anajua kwamba ushindani ni mkubwa nasi tunahitaji kupata matokeo mazuri.
"Malengo yetu ni kuona kwamba tunapambana ili kupata ushindi na kufikia malengo ya kutwaa ubingwa," .
0 COMMENTS:
Post a Comment