KIKOSI cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morroco leo Aprili 10 kimekwea pipa kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudio wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Nkana FC.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Namungo 0-1 Nkana FC jambo lililowafanya wawakilishi hao wa Tanzania kimataifa kuyeyusha pointi tatu muhimu.
Kwenye kundi D Namungo FC ipo nafasi ya nne ikiwa haijakusanya pointi baada ya kucheza mechi tatu zote imepoteza.
Nkana ipo nafasi ya tatu na ina pointi 3 ilizipata mbele ya Namungo FC. Kinara wa kundi hilo ni Raja Casablanca mwenye pointi 9 kati ya hizo tatu alizichukua kwa Namungo na nafasi ya pili ni Pyramids yenye pointi 6 ambayo nayo ilishinda mbele ya Namungo.
Morroco ameweka wazi kwamba kinachowashinda wachezaji wake ni kutumia nafasi pamoja na uzoefu jambo ambalo analifanyia kazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment