Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amezitaka timu za Yanga na Namungo kuiga mfano wa timu ya Simba katika kutangaza utalii wa Tanzania kupitia jezi zao ambazo zimeandikwa Visit Tanzania.
Ndumbaro amesema kuwa wao hawachagui timu yoyote ya kufanya nayo kazi ,kwahiyo waliopo tayari wakaribie ofisini kwetu ili waweze kuitangaza Tanzania kitaifa na kimataifa.
Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika wapo hatua ya robo fainali katika ligi hiyo yenye ushindani ambapo ilikuwa inavaa jezi zenye neno Visit Tanzania.
Ndumbaro amesema:"Simba ndiyo walikuja kuomba nafasi hiyo na wala hatujawapa pesa wanatangaza bure hivyo timu zingine zisiogope kuja hii ni fursa ya kutangaza utalii wa nchi yetu, " amesema Ndumbaro.
Namungo inapeperusha bendera katika Kombe la Shirikisho ikiwa ipo hatua ya makundi, Yanga kwa sasa inapambana kutwaa taji la ligi ili iweze kurejea katika mashindano ya kimataifa.
Aanze na Taifa Stars, Ngorongoro heroes nk
ReplyDelete