KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, ameweka hadharani kwamba anachokitaka kukifanya ndani ya timu hiyo ni kuwabakisha mastaa wake wote kwa misimu minne ijayo kwa ajili ya kuifanya timu hiyo ifanye vizuri kwenye mechi za kimataifa.
Gomes ameongeza kwamba anataka kuwabakiza nyota wake mbalimbali ndani ya kikosi hicho kutokana na kuwapenda lakini kujenga timu bora zaidi ndani ya Tanzania na nje kwenye michuano yao ya kimataifa.
Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema kuwa: “Sijui kuhusu wao kuondoka lakini nasema nawapenda wachezaji wangu, nahitaji kubakia nao kwa misimu mingi ijayo. Ni jambo zuri kutengeneza timu nzuri kwa misimu mingi ijayo.
“Nataka niwe nao wote kwa misimu miwili, mitatu au minne ijayo kwa ajili ya kujenga timu bora zaidi. Nina wachezaji wazuri lakini wanatakiwa kuboresha zaidi jinsi tunavyocheza. Najivunia kufanya kazi nao," amesema.
Simba imetinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni namba moja kwenye kundi A baada ya kufikisha jumla ya pointi 13.
Miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa wakitajwa kuhitajika na timu nyingine ni pamoja na Luis Miquissone ambaye anatajwa kuwekwa kwenye rada za FC Platinum, Al Ahly na Al Merrikh.
Usije ukawaacha na kwenda kutafuta malisho mazuri wao wakabaki na njaa
ReplyDeleteMfaransa anataka kuwapa kihoro matopolo yaani miaka mine ijayo bila ya ubingwa.. Na kutokana na kiwango na utulivu uliopo hayo yanawezekana kabisa
ReplyDelete