April 12, 2021

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa wakati wa timu ya Simba kwa sasa umefika kukaa kileleni katika Ligi Kuu Bara kwa sababu wamemaliza mechi zao za kimataifa hatua ya makundi hivyo wana muda wa kucheza mechi za ligi.

Kwa sasa kinara wa Ligi Kuu Bara ni Yanga wakiwa na pointi 51 baada ya kucheza jumla ya mechi 24.

Simba ipo nafasi ya tatu na pointi 46 baada ya kucheza mechi 20 nafasi ya pili ipo mikononi mwa Azam FC wenye pointi 47 baada ya kucheza mechi 25.

Gomes amesema:"Tulikuwa na mechi za kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ila tayari tumeshakamilisha mechi hizo na tumefurahi kuona kwamba tumefika hatua ya robo fainali.

"Kutimiza lengo la kwanza inamaanisha kwamba tutakuwa na muda wa kucheza mechi zetu ambazo ni za ligi hasa ukizingatia kwamba hatutakuwa bize katika mashindano ya kimataifa.

"Huu sasa utakuwa wakati wetu wa kuweza kucheza mechi zetu kwa kuwa wachezaji ni wazuri na wapo tayari itakuwa ni nafasi yetu kuweza kuongoza ligi," .

Aprili 14, Uwanja wa Mkapa ni Simba inakibarua cha kusaka ushindi mbele ya Mtibwa Sugar, mchezo wao wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma, Mtibwa Sugar 1-1 Simba, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic