April 14, 2021


 STAA wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi, amesema wala haitashangaza kuona timu hiyo ikitinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu na kulichukua kombe.

 Okwi ambaye alitamba na Simba, huku pia akipita Yanga, ameitaja Simba kuwa ni moja kati ya timu bora Afrika kwa sasa na imecheza kwa kiwango cha juu sana msimu huu na wanastahili kupata mafanikio makubwa.

 

Kauli ya Okwi imekuja wakati huu ambao Simba imetinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa kinara wa Kundi A mbele ya Al Ahly.


Okwi amesema:-“Simba wanamshangaza kila mpenda soka kwa sasa Afrika, kitendo cha kumaliza kundi wakiwa vinara mbele ya timu kama Al Ahly na AS Vita siyo jambo dogo, hiyo inaonesha kuwa wapo imara na ni timu bora kwa sasa Afrika.


 


“Haitashangaza kuona wanacheza fainali na hata kuchukua kombe lenyewe, wanastahili kupata mafanikio makubwa msimu huu kutokana na jinsi kikosi chao kilivyo bora.

 

“Tanzania kwangu naona ni kama nyumbani kwa sababu nimeishi na watu wake vizuri, halafu ninaipenda sana hasa klabu yangu ya Simba ambayo nilicheza kwa muda mrefu.

 

 “Ninaipenda kwa kuwa ndiyo imebadilisha maisha yangu katika sehemu kubwa, lakini pia imenipa heshima hadi hapa ambapo nimefika, hivyo najivunia kuipenda Simba," .

 

 Kwa sasa Okwi anakipiga kwenye timu ya Al Ittihad Alexandria inayoshiriki Ligi Kuu Misri, Ijumaa, Aprili 9 alikwenda jijini Cairo kuishuhudia Simba ikicheza na Al Ahly kwenye mchezo ambao Simba walifungwa 1-0.

 

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic