JUNIOR Lokosa, mshambuliaji aliyesajiliwa na Simba kwa ajili ya mashindano ya kimataifa amepata warithi wake kwenye Ligi ya Mabingwa ambao ni Chris Mugalu, Meddie Kagere na John Bocco.
Lokosa raia wa Nigeria alisajiliwa na Simba akitokea Klabu ya
Esperance ya Tunisia Januari, mwaka huu ila kwa sasa tayari ameshasepa Bongo
kutokana na uwezo wake kuwa chini ya matarajio ya benchi la ufundi la Simba.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Mkuu wa Simba, Didier
Gomes, raia wa Ufaransa alisema kuwa hana mashaka kuhusu kutokuwepo kwa Lokosa
kwa sababu anao wachezaji wengine katika nafasi hiyo.
“Kwa kweli nimezungumza sana kuhusu Lokosa,(Junior) ila ngoja
niweke wazi kuwa kwa nafasi ambayo anacheza wapo wachezaji wenye uwezo wa
kufanya vizuri, yupo Mugalu, (Chris), Kagere, (Meddie) na Bocco, (John).
“Kikubwa ambacho ninafurahi ni kwamba wachezaji wote waliopo
wanafanya kile ambacho ninawaelekeza na wanakifuata kwa wakati,” alisema
Gomes.
Hapo ndo Kiswahili kinapokuwa kigumu, wanarithije mikoba ya Lokosa wakati Lokosa hakuwahi kuwa na nafasi Simba!
ReplyDeletehv hii blog wanaoandika habar ni wamesoma kweli? kichwa cha habar tofqut kabisa na habar
ReplyDeleteHawana kitu cha maana cha kuripoti na hivo kupelekea kuandika utumbo. Tuwasamehe bure
ReplyDeletePumba tupu wanalisi vp sasa
ReplyDelete