THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kwa sasa timu hiyo inahitaji maombi kutoka kwa wadau pamoja na mashabiki ili itimize lengo la kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 24 ambazo ni dakika 2,160
imekusanya pointi 24 ina wastani wa kukusanya pointi moja kila baada ya dakika
90 ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kifaru amesema kuwa hawapo
kwenye nafasi nzuri kwa wakati huu kutokana na matokeo yasiyoridhisha licha ya
kuwa na kikosi bora.
“Tumekutana na kimbunga kwa sasa ambacho ni cha ajabu kwetu,
tunahitaji maombi kutoka kwa wadau pamoja na mashabiki ili tuweze kutimiza
malengo yetu ya kubaki ndani ya ligi hii ambayo tuna historia nayo nzuri.
“Unajua ukisema kwa sasa Mtibwa Sugar ishuke sasa hapo nani
ambaye ataleta ushindani kwa timu nyingine ambazo zinafanya vizuri? Pale ambapo
tumekosea benchi la ufundi linafanyia kazi kisha tukiweza kupata ushindi kwenye
mechi zetu tuna imani kwamba tutabaki,” amesema.
Baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 5-0 dhidi ya Simba Uwanja
wa Mkapa, leo ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar, Uwanja
wa Jamhuri, Morogoro.
0 COMMENTS:
Post a Comment