April 25, 2021

 


AZAM FC inaayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina leo Aprili 25 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kipindi cha kwanza timu zote zilitoshana nguvu na kuwafanya waende vyumba vya kubadilishia nguo ubao ukisoma Yanga 0-0 Azam FC.

Ni Prince Dube dakika ya 85 alipachika bao la ushindi nje ya 18 na kumfanya afikishe jumla ya mabao 12 akiwa ni kinara kwa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara.

Ushindi huu unaifanya Azam FC kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wao uliopita ambapo walifungwa bao 1-0.

Kwenye msimamo Azam FC baada ya kucheza mechi 28 inafikisha jumla ya pointi 54 ikiwa nafasi ya tatu huku Yanga ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 27 nafasi ya pili na kinara wa ligi ni Simba mwenye pointi 58 baada ya kucheza mechi 24.


11 COMMENTS:

  1. Mwandishi umechemsha, ni Azam dhidi ya Yanga na si Azam dhidi ya Azam,tafadhali kuweni makini sana,makosa yenu ni mengi mnooo kila wakati.

    ReplyDelete
  2. Jamani dube hafungi ramadhani lkn sio hafungi magoli

    ReplyDelete
  3. basi Yanga wakamnunue Dube badala ya Zimbwe? habari ya Ubingwa sahau...Ilikuwa Simba akifungwa mechi tata na Yanga ashinde zote..Sasa ni Yanga ashinde 7 na Simba afungwe 4 ...ni hapo tu Yanga atakuwa bingwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shibeni maneno ya mawakala naona hamchoki kuingizwa chaka

      Delete
  4. Ngoja nikusahihishe mdau,yanga kabakisha mechi 7,Simba kumi,katika hizo Simba akishinda 6 na droo moja,Simba bingwa mara nne in row,Simba hii haifugiki,Utopolo nafikiri kesho watasema wanajitoa league kuu,maana walisema iwe mvua au jua mwaka huu kombe ni lao wakati Simba anajiandaa kuingia semi final ya Caf champion league.Mimi nafikiri wadau wangu wa Simba,nchii hii Simba Hana mpinzani na tuache kujibishana na Utopolo because they are not our level,arch rival wetu watabaki As Vita,Al ahly,mazembe,Kaizer chiefs na other African club Giants,wakubali wakatae.Sisi fans of Simba tuache kufikiria ubingwa wa Vodacom Kama Utopolo maana huo ni wetu,tufikirie Ubingwa wa Africa.Simba baba lao,Simba oyeeeeeeeere

    ReplyDelete
    Replies
    1. Caf mmeshafika mwisho wa kupenyeza

      Delete
    2. Ujue bado pointi 3 Azam awashushe.., Na Simba ikishinda viporo vyake vitatu itawazidi pointi 10 na magoli ya kufunga zaidi ya dazeni moja.. Je unajua katika timu 8 zilizofuzu robo fainali ni Simba inaongoza.. sawa iweje ndiyo wamefika mwisho. Wivu tu

      Delete
  5. Utopolo Prince anasemaje? NDIO maana hamufanikiwi mme focus sana kwenye mambo ya Simba.Bado twrehe 8.

    ReplyDelete
  6. laana ya kutokuwa na fadhila..jana Mwambusi hakuwepo kwenye benchi ya ufundi..kawaida ya utopolo kukosa fadhila..alifanyiwa Mkwasa hivyo hivyo walipomleta Eymael..mwaka juzi walipata fursa ya kucheza CAF ingawa walikuwa hajachukua ubingwa wala FA Cup..kipindi chote kwenye mashindano walichelelea matokeo ya Simba kutolewa na UD Songo..matokeo yake wakajifunga wenyewe na kujiondoa mashindanoni kule Zambia

    ReplyDelete
  7. Teh teh teh teh!!!!!uketo unaliwa na wenye meno Yao jamani,kwann mnampa kikongwe?????hamjamtendea haki kabisa hatimae mmemlaizia gego lake moja lililobaki,huu sio uungwana,ahsante mkaanga uketo.

    ReplyDelete
  8. Na bado next stop kuna Prisons katika FA cup pale Nelson Mandela, kuna mechi ya Simba na Namungo kule kwao..Asipoangalia huyo Nabii atapigwa mechi zote nne mfululizo! mmrudisheni kikongwe au Mkwasa waokoe jahazi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic