AZAM FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kwa sasa imeanza kuivutia kasi KMC kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, ubao ulisoma KMC 1-0 Azam FC na kuwafanya wana Kino Boys kusepa na pointi tatu za wana pira Ice Cream.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Mei 15 ambapo Azam FC itakuwa nyumbani kupambana kusaka pointi tatu.
Kwenye msimamo wa ligi, Azam FC ipo nafasi ya tatu ina pointi 54 inakutana na KMC iliyo nafasi ya tano na pointi 41 zote zikiwa zimecheza jumla ya mechii 28.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa hesabu za timu hiyo ni kupata pointi tatu kwenye mechi zao zilizobaki ili kuweza kutimiza jambo lao.
"Bado tupo na kazi ya kufanya, tunakusanya kwanza pointi katika mechi zetu kisha tutakaa baada ya ligi kuisha na kujua ni kitu gani ambacho tumekusanya, lengo lipo palepale," amesema.
Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa watawafuata wapinzani wao kwa hesabu za kuyeyusha Ice Cream za Azam.
0 COMMENTS:
Post a Comment