May 22, 2021


BENCHI la ufundi la Yanga limewataka mashabiki kutulia na kusubiri matokeo chanya kwa kuwa wapo imara na watafanya vizuri katika mechi zao ambazo zimebaki.

 Hiyo ni baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara walipocheza dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

 

Timu hiyo hivi sasa ipo katika maandalizi ya mchezo wa Kombe la FA watakaocheza Jumanne ijayo dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga. 


Kocha wa makipa wa timu Razack Siwa amesema kuwa kadiri ya siku zinavyokwenda anaona mabadiliko ya kikosi chake kutokana na kucheza kwa kufuata maelekezo anayowapa mazoezini.


Siwa amesema kuwa bado anaendelea kuyafanyia baadhi ya maboresho ikiwemo safu ya ushambuliaji. Aliongeza kuwa ana matumaini makubwa ya timu yake kupata matokeo mazuri sambamba na vijana wake kucheza soka safi la kuvutia kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki.

 

“Kikubwa mashabiki wanatakiwa kuwa na subira kwani bado kocha ni mpya, hivyo ana sera yake ya aina ya uchezaji.


“Hakuna kitakachoshindikana, hivi sasa tunaboresha baadhi ya nafasi ikiwemo ya ushambuliaji, hivyo mashabiki waondoe hofu wajiandae kupata furaha katika michezo ijayo ya ligi ya Kombe la FA.

 

“Mabadiliko yameanza kuonekana katika michezo iliyopita ukiwemo dhidi ya JKT Tanzania, kila shabiki ninaamini alifurahia kuona vijana wakipambana huku wakicheza soka safi la kuvutia,” amesema Siwa.

9 COMMENTS:

  1. Wanaanza kujiamini baada ya kupata uchochoro wa kupitisha milungula, ngoja iko siku watakamatwa, prison chupu chupu kumbe hawajakoma

    ReplyDelete
  2. Wewe nadhani Timu unayoongoza kwa kufisadi Mpira hapa bongo inajulikana mikia Fc kuanzia Kacheka mpaka Timu yenyewe mnatisha mpaka aibu .na imekuwa Utamaduni wenu wa Kudumu hata Timu ndogo lazima mpenyeze

    ReplyDelete
  3. Ndiyo maana mmejijaza TFF mpaka wafagia Choo utafikiri hakuna kazi zaidi ya Mpira ,usirudie kutwambia tunatoa Mlungula hapa ni Yale ya nyani hajui kundule paka shume jeusi Tena.

    ReplyDelete
  4. Simba katika Mechi kumi ushindi wa kweli ni tano nyingine Mpira wa bar tu.

    ReplyDelete
  5. BWache wajidanganye na kuwadanganya wenzako maana tangu kupata hivo vieili hawaoni hawasikii

    ReplyDelete
  6. Timu iliyo na rekodi ta rushwa hapa Tanzania na kiongozi wao kufungiwa ni Yanga. Katibu mkuu wao aliyefungiwa maisha kwa kuhonga waamuzi kutoka Ethiopia kabla ya mechi yao na Gor Mahia kwenye michuano ya CAF.Makongoro alifungiwa maisha.Ndio timu pekee.

    ReplyDelete
  7. Katibu mkuu huyo ni Issa Makongoro. Wengine hapa walikuwa hawajazaliwa au ni wakuja walikuwa hawajaja mjini.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic