JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union ya Tanga amesema kuwa anaamini kuwa watabaki ndani ya Ligi Kuu Bara licha ya kuwa kwenye mwendo wa kusuasua.
Mgunda amekiongoza kikosi cha Coastal Union kwenye jumla ya mechi 28, alishinda 8, sare 9 na kupoteza 11 huku kikosi kikiwa nafasi ya 11.
Mgunda anashikilia rekodi ya kuwa kocha wa kwanza msimu wa 2020/21 kushinda mbele ya Yanga kwa ushindi wa mabao 2-1 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa kwa sasa wanazidi kujipanga kwa ajili ya mechi zao zilizobaki na watabaki ndani ya ligi.
“Bado tunapambana kwa sasa kwa kuwa tupo kwenye maandalizi na ligi ipo wazi kwamba inajulikana ni ngumu nasi pia tunapambana ili kupata matokeo chanya.
"Hatupo kwenye mashindano mengine kwa sasa zaidi ya ligi na vijana wapo tayari kwa ajili ya ushindani hivyo nina amini kwamba tunaweza kufanya vizuri na tupo tayari," amesema.
Kwenye Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora ilitolewa na Mwadui FC kwa kufungwa mabao 2-0.
Mchezo wake ujao wa ligi ni dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa Mei 11, Uwanja wa Mkapa, ule wa mzunguko wa kwanza walipokutana ubao ulisoma Coastal Union 0-7 Simba.
Hivyo utakuwa ni mchezo wa kisasi kwa Coastal Union kwa kuwa ilipoteza pointi tatu mchezo wa kwanza itahitaji kuzirejesha. Itakuwa inapambana kubaki ndani ya ligi hukus Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 61 inawania kutetea taji la ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment