UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba nyota wao wawili wamerejea kikosini kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Simba.
Mchezo huo wa Kariakoo Dabi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 8 ambapo timu zote zimekuwa zikitamba kwamba zitaibuka na ushindi ili kusepa na pointu tatu mhimu.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa maandalizi pamoja na mipango inakwenda vizuri hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi kila kitu kitakuwa sawa.
"Wachezaji waliokuwa majeruhi tayari wamerejea. Dickson Job pamoja na Abdalah Shaibu, 'Ninja' walikuwa na maumivu ila kwa sasa wanaendelea vizuri na wamerejea.
"Kuhusu maandalizi kiujumla yanaendelea vizuri hivyo mashabiki wasiwe na mashaka tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya watani wetu wa jadi ambao ni Simba," amesema.
Job na Ninja hawa wote ni mabeki ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi, tayari wameanza mazoezi kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo wenye ushindani mkubwa.
Kwenye safu ya ulinzi, Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 27 imeruhusu mabao ya kufungwa 17 inakutana na Simba ambayo imeruhusu jumla ya mabao 10 katika mechi 25.
Waje tu msijepata kisingizio
ReplyDeleteHuyu anatunga story hili wapangwe ,mabeki wa YANGA wote Kama ngome ya Kandahari watu wa kupasua mjiandae
ReplyDeleteNi either Ninja vs Mwamnyeto au Ninja vs Lamine ,Job anacheza namba sita (Ikuta wa wa2 watatu Kati /mbele Sarpong ,Yacouba na Nchimbi Kati Fri na Mkoko ,sub Tuisila,Saido ,Mauya ,Defenders na Mauya z hapa ni Mpira speed nguvu na tunamwonya Refa Hatutaki Umayai
ReplyDeleteUSiogope sheria za soka hazichagui mechi, mkileta uninja penati Kama kawaida... Mpira sio ugomvi Ila ni burdan
DeleteFri ni Fei na Mukoko
ReplyDeleteManula, Kapombe, Zimbwe, Wawa, Onyango, Lwanga, Miqueson, Morison, Bwalya, Chama, Mugalu...Sub Kakolanya, Mkude, Mzamiru, Kennedy, Nyoni, Bocco, Kagere... Uto Mkipata hata sare pongezi kwenu
ReplyDelete