HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa anaweza kucheza kama kiungo wa Yanga Carlohs Carlinho na akamzidi kutokana na uwezo wake.
Manara amesema kuwa anaweza kufanya hivyo ikiwa atakuwa anakaa peke yake kama ambavyo anafanya mchezaji huyo raia wa Angola ambaye kwa sasa anasubiri ripoti kutoka kwa madaktari ili kujua hatma yake ya kuweza kuivaa Simba Mei 8, Uwanja wa Mkapa.
Manara amesema:"Unajua huwezi kuwa mchezaji, kiungo kila wakati unapiga tu pasi, kuna wakati kiungo mechi ishachafuka haiwezekani, unauchukua kama Chama, (Clatous) vile anaukata katikati namna hii.
"Mimi na uzee huu na miaka 40 na.. ninaweza kucheza kama vile ambavyo Carlinhos anacheza, mimi ninacheza.
"Kuzima na kupasi hiyo nacheza. Hakuna bingwa wa pasi duniani kama mimi, yaani nazima napasia nazima napasia ilimradi nakaa eneo la peke yangu," .
Mchezo wake wa mwisho kucheza Carlinhos ilikuwa ni mbele ya Tanzania Prisons ambao ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho.
Wakati ubao ukisoma Tanzania Prisons 0-1 Yanga alitumia dakika 64 na kupata maumivu jambo lililofanya asiyeyushe dakika zote 90.
Mtindo wake wa kucheza ndani ya uwanja ni ule wa pasi moja akipata anaaachia kwa wachezaji wenzake ndani ya uwanja.
Rekodi zinaonyesha kuwa ana pasi tatu za mabao kwenye ligi na amefunga mabao matatu pia.
Hapa shida ni barehe zilizopitiliza ,Elimu ndogo,mnajiita Waandishi unaleta mahaba ya kwako ,unachomekea Manara na Kama kweli kasema utu uzima wake,angekuwa akati mauno hadhari .
ReplyDeleteHadharani
ReplyDelete