May 6, 2021

 


KUELEKEA kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi unaotarajiwa kuchezwa Mei 8, Yanga wamesema kuwa watani zao wa jadi Simba watawafunga wengine ila sio wao.

Mchezaji wa zamani wa kikosi hicho ambacho kwa sasa kinanolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi, Mwanamtwa Kiwelu amesema kuwa wapo vizuri na watawafunga Simba.

 "Wapenzi wa Yanga wasiwe na wasiwasi sisi tupo wazima hatuumwi, hao Simba hatuna matatizo nao waje na tuna hasira nao, watawafunga wengine ila sio sisi, sisi tupo vizuri na tuna hasira nao," amesema.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa utatoa picha ya bingwa wa ligi kwa msimu wa 2020/21 ambao umekuwa na ushindani mkubwa.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 27 na Simba ipo kwenye nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 61 kibindoni.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, kwenye mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Ni Michael Sarpong alitupia kwa Yanga kwa mkwaju wa penalti na kwa Simba ni Joash Onyango ambaye alipachika bao hilo kwa kichwa.  

1 COMMENTS:

  1. Huu weledi wa hawa makanjanja wa hii blogu.Sasa huyu Kiwelu anacheza namba ngapi?Anaiwakilisha Yanga kama nani?Ushabiki wa kijinga tu.Tuleteeni uchambuzi wa maana sio ujinga ujinga tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic