KUFUATIA kuahirishwa kwa mchezo kati ya Simba na Yanga uliotakiwa ufanyike juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, hatimaye uongozi wa Simba umetoa tamko rasmi ukizitaka mamlaka ziwashushe madaraja mawili Yanga.
Taarifa za jana Jumapili kutoka katika Kitengo
cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba,
ilisema:-“Sote tunajua kitendo kilichofanywa na Yanga
tafsiri yake ni kwamba wamegomea mchezo na
adhabu yake ni kushushwa madraja mawili na Simba kunufaika kwa kupewa alama tatu na mabao mawili.
“Mbali na hayo, pia kitendo chao ni sawa na usaliti kwa nchi na Serikali ambayo ilitoa maelekezo maalumu kusogezwa mechi kwa saa mbili zaidi.
“Hivyo basi kwa upande wetu tunaamini ahirisho lile la mechi limefanywa makusudi na Bodi ya Ligi kwa nia ya kuipendelea Yanga ambayo ilipaswa itii maagizo yao na ya TFF juu ya muda wa kuanza kwa mechi kama ilivyoelekezwa na Serikali na kisha kutujulisha
sisi.
“Simba imesikitishwa sana na uamuzi huo wa
Bodi ya Ligi ambao unaonyesha dhamira ovu
juu ya klabu yetu na jambo jingine linaongeza mashaka juu ya kadhia hii ni kuiruhusu Yanga kuingia uwanjani kinyume na utaratibu wa muda maalumu unaoruhusiwa kabla ya kuanza kwa mchezo husika.”
washushwe tu! hawafai!wakishinda ni kwa vile kanuni zimekiukws. Wakati wa Malinzi na TFF yake waliwahi kuwa bingwa kwa sababu kanuni
ReplyDeleteinayosema mchezaji anapokuwa na kadi 3 za njano hapaswi kucheza. Endapo kanuni ingefuatwa Simba ilipocheza na Kagera Sugar, basi Simba angepata pointi tatu na angemzidi Yanga na kutwaa ubingwa..Ile kanuni ilitupiliwa mbali.Laaana ya kutofuata kanuni inatenda haki.Na sasa miaka minne sasa ukame wa ubingwa na sana sana ni ubingwa wa Mapinduzi..
Haki husikia kilio...kufanya mamilioni ya watu kusubiria mechi, maelfu zaidi ya 40 kununua tiketi na wengine wengi kusafiri Dar, halafu viongozi hawawezi vumilia masaa mawili, na ipo kanuni inayoruhusu kulalamika.
Kanuni isiwe muda tu, ni kanuni gani kumng'ang'ania Morrison,haki za Tambwe, Kakolanya, na wengine wengi!ukweli na haki vipo.