May 10, 2021

 


GUMZO kubwa kwa sasa katika mpira wa 
Tanzania ni kuahirishwa kwa mechi ya watani Simba na Yanga, mechi ambayo ilipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, juzi Jumamosi.


Mechi hiyo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu, Simba wakitaka kujikita kileleni zaidi huku Yanga wakitaka kupunguza pengo la pointi nne kwa kuwa wao wanazo 57 na watani wao wana 61.


Kila shabiki alikuwa anaamini ni wakati mwafaka wa kikosi chake kufanya kweli, Simba wakijivunia ubora wa kikosi chao na Yanga wakielezea ubabe wao kwa Simba.


Ilikuwa ni raha ya ushindani karibu wiki nzima za tambo za watani wa jadi, mechi hiyo maarufu kama Kariakoo Dabi ambayo mwisho wake imeishia hewani.



Kilichosababisha mechi hiyo kuahirishwa ni agizo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) wakalitekeleza.


Agizo halikuwa kuahirisha mechi, agizo lilikuwa ni kusogeza mbele mechi kwa muda wa saa mbili pekee na baada ya hapo kipute kingepigwa. TFF na TPLB walipanga mechi ichezwe saa 11 jioni, lakini siku hiyohiyo wakapata agizo la wizara kwamba mechi hiyo itapigwa saa 1 usiku. Saa mbili mbele ya muda waliokuwa wamepanga.


TFF kupitia TPLB, wakawataarifu wadau wao Simba waliokuwa wenyeji na Yanga kwamba mambo yatakuwa hivi.

Wakayapokea lakini mwisho tumeona Yanga waliamua kutoa timu uwanjani tayari mashabiki wakiwa wameingia uwanjani mapema.


Maswali ni mengi sana, kwamba vipi wafunge safari hadi uwanjani na baada ya hapo watoe timu kwa kusogezwa saa mbili mbele? Kuna jambo gani linawafanya Yanga kuwa katika uamuzi huo, tuwaachie wenyewe kwanza na ninaamini watalimaliza vizuri ingawa busara ya kuangalia usalama wa mashabiki, haikuwa imetumika na badala yake ulikuwa uamuzi wa kishabiki.


Ukiachana na hilo vizuri tukaliangalia katika sura ya pili, kuwajalidi TFF ambao wamekuwa wakishambuliwa na kufikia hatua ya viongozi wao kudhalilishwa.


Najua wapo watu huona au kuamini silaha yao ni matusi, huamini kutukana ndio jambo sahihi au ndio ujengwaji wa hofu au ndio uchambuzi wa jambo fulani lakini ukweli ni hivi, unayeona anatukana tu, anakuwa na uwezo mdogo sana wa ufikiri.


Hapa TFF unawalaumu wapi na kufikia kuwadhalilisha, agizo limetoka wizarani ambayo ni Serikali ya nchi yetu, wao wanaweza kupinga vipi? Lakini nani anajua Serikali iliamua hivyo kwa sababu zipi za msingi kwa kuwa kila mmoja anasema lake?

Kama ni suala la kiusalama je? TFF wanaweza vipi kuipinga Serikali? Katika taarifa yao, TFF wamesema

wamefikia uamuzi huo baada ya kupokea agizo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hii nayo haieleweki hadi watu kuelekeza ncha ya kisu kwao na kuwashambulia bila sababu za msingi.


Inawezekana ukawa fundi sana wa kulaumu, fundi sana wa matusi lakini basi jifunze hata kusoma na kuelewa halafu ukajenga hoja zako na watu wakakuelewa.

Yanga walifuata kanuni, TFF wakafuata agizo la Serikali, tujadili katikati ya hapo, nini kingetumika, weledi, busara, mihemko?

Lakini si mashambulizi tu kwa TFF kwa kuwa ndio mazoea. Vizuri kuifanya mijadala ya mchezo wa soka ikawa inayozalisha au kufundisha badala ya mihemko na kukurupuka kuwa ni sehemu ya mijadala ya mchezo wa mpira au kutengeneza picha eti watu wa mpira wako.

23 COMMENTS:

  1. Yaan mwandishi unazngumza Kama hujakaa darasan . Sasa so useme tu yanga wamefanya makosa maana ndicho unachotaka kutuaminisha

    ReplyDelete
  2. Hii busara inayozungumziwa haiangilii nini madhara kwa mashabiki wanayoyapata kwa kupotezewa muda

    ReplyDelete
  3. Hata hoja zimekaaa kishabiki kufukia kila siku maovu yaendelee busara unaiona kwa yanga tu watanzania tumezidisha ushabiki wa kinafiki na waandishi Kama huyu n
    do wanatuhalipia tasinia ya mpira wa n'chi hii

    ReplyDelete
  4. Hivi mbona unakuwa kama si mataalam wa michezo! Hivi kanuni na taratibu za kuahirisha mechi zikoje? Ukipata jibu utafaham ukweli

    ReplyDelete
  5. Kanuni hizo mbona hazijatumika kwenye mechi za Azam, Biashara na Gwambina dhidi ya Yanga?Kwanini Kanuni hizo hazijatumika kwenye mechi za Simba dhidi ya Mtibwa na Dodoma Jiji?Mechi zote hizo zilibadilishiwa muda. Kanuni kwa timu hizi 2 tu.Tokea ligi ianze Yanga na Simba wamecheza mechi saa 8? KANUNI hiyo ys ratiba haiwahusu? Tuache unafiki wa kusifia ujinga ujinga.Mbona hao wachambuzi uchwara hawajiulizi hilo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwanza nishukurubkwa uzima pili tubadilikeni jamaji asikari mzuri ni yule mwenye kutii maelekezo ya mkuu na piya embu yanga kabla ya kuangalia kanunu ya 15 wangelipitia na kanuni ya 20 na 21 kwa nini wanazisoma kanuni robo robo wa maleze kanuni mwanzo mwisho kisha naamini gemu lilikuwa lipigwe bila hofu

      Delete
  6. Hata serikali ikivunja sheria kanuni na taratibu tukubali tu? Wewe kiazi kabisa busara si kuvunja sheria kanuni na taratibu tulizojiwekea.

    ReplyDelete
  7. Hapo tatizo ni yanga, mengine ni kupoteza muda tuu. Nani alishawahi kuwa kiongozi wa taasisi ya umma na akapewa maagizo akayapinga? Msiongee tuu kama mazuzu. Agizo lilikuwa kusogeza muda wala sio kuahirisha, wangecheza under protest. Tatizo wanategemea mchawi wao kasemaje, aliriga muda wa saa 11 ikawa ngumu saa 1. Hsta hiyo saa 11 wangefungwa na litimu lao bovu, msijifanye mnajua sana sheria chezeni mpira.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watu wa simba bhana, wakati wa sakata la Morisson sheria zilikiukwa na alawa guru, lakini kwenye kuahirisha mechi kanuni isitumikebila busara, basi busara ingetumika hata kwenye sakat la Morisson. Mpira ni mchezo unaoendeshwa kwa sheria na kanuni.Kama hivo ndivyo kanuni ni lazima zifuatwe kama vipi sheria na kanuni zote za mpira zifuatwe tutumie busara tu

      Delete
  8. Hivi unataka busara ipi? Kwani hiyo busara ndo kanuni za ligi acheni kutetea undezi na kujipendekeza kwani wao waombe radhi na anastahili kujiudhuru wote hao serikali,tff,bodi ya ligi ndo maana manara kawabatiza Jina la

    ReplyDelete
  9. Hivi mwandishi tuambie pengine mwenzetu umeambiwa sababu yenye mashiko ya kuhairishwa mechi ambayo ata Waziri Mkuu wakati anahutubia Bunge inaonyesha inaonyesha haijamwingia?

    ReplyDelete
  10. Tukitaka kwenda mbele tuache sheria,kanuni na taratibu zifuate mkondo aliyesababisha hili tatizo ahukumiwe kwa taratibu hizo hizo.Mambo ya busara hayana nafasi hapa.

    ReplyDelete
  11. Waafrika bhana tuna matatizo sana ndo mana hata Trump alitusema sana, ukweli ni kwamba simba baada ya paka wao kugoma kuingia uwanjani ikabidi wawaombe tff kusogeza game mbele maana wameona watagongwa hivo wapewe masaa 2 wakafanye mambo yao, wanawasingizia tu bure wizara

    ReplyDelete
  12. Hapa shida ya Hawa jamaa Usimba umewazidi,na hapo ndipo mtajua uadirifu huyu Mwandishi anajulikana na ni mpenzi wa Simba,yaani kwa akili yako Makosa ya TFF unayapeleka Yanga the so called Busara kwanini hakikuwaongoza wale waliosogeza muda

    ReplyDelete
  13. Hiyo busara ni kwa vilabu tu. Je hao TFF na TPLB walitumia busara? Ni mara ngapi vilabu vimepigwa faini na adhabu nyingine kwa kukiuka kanuni. Je kuna vyombo vikikiuka kanuni ndipo busara itumike? Mwandishi umeandika kwa mahaba na mihemko. Rudi darasani kajitunze upya kubalance kalamu yako

    ReplyDelete
  14. Mwandishi huyu ni kiazi kabisa. Kama ulitaka busara itumike kwa nn waliotoa tangazo la kuahirisha mechi masaa 2 kabla wasingetumia busara kwanza kwa kuzingatia kwamba tayari karibia mashabiki wote walikuwa wako uwanjani. Lakini kuonyesha kwamba mwandishi huyu hajitambui hata akakurupuka kutoa makala hi angesubiri kwanza kusikia maamuzi ya Serikali leo yanasemaje ndo angekuja na malalamiko yake ya mahaba. Sasa serikali imetoa majibu na hakuna upande wowote ilioulaumu kwa sababu imepima ikaona mazingira Yale na kwa ukubwa wa mechi ile ikaona kila upande waliamua kulingana na walichokiamini hata Kama Serikali ndio waliotoa agizo

    ReplyDelete
  15. Simba wamebebwa ili wacheze vyema mechi yao na Kaizer Chief. Huu ndio ukweli kama wangecheza na Yanga morali ingepungua na hofu ya wachezaji kuumia. Huu ndio ukweli ambao unafichwa kusemwa - Sasa viongozi lazima wawe wa kweli na wasitumie kivuli kusema vyenginevyo.

    ReplyDelete
  16. Ukweli mwandishi Kuna kitu alitaka kuandika lakini hakuwa tayari na hakujiandaa kufikisha ujumbe halisi, nafananisha na safari ambayo ukijianda na kwenda sehemu bila kujua unaenda kufanyanini, naamini mwandishi kile anachoaminijambo hili limefanywa kwa sababu ya ushabiki na mihemuko basi hata mwandishi kuangukia humohumo kwenye ushabiki na mihemuko
    Kuhusu busara ni kweli ingetumika na mashabiki wakapata kile walichotarajia lakini katika wakati na muda sahihi ambao ulipangwa awali, Je mwandishi anajua watu wana Familia zao na majukumu akumbuke Kuna watu walifika uwanjani mapema sana wakitegemea watatoka mapema na kuwahi Familia zao majumbani... Mwandishi anatuaminisha kuwa kanuni zivunje kwa sababu serikali imesema, Nani anajua utaratibu katika ya TFF na Serikali na yupi aliyetakiwa kumshauri mwingine kuhusu kanuni za soka
    Kuhusu dharula ni ipi ambayo ilitaka mechi isogezwe hakuna anayejua!
    DOKEZO:SOKA LINAENDESHWA KWA SHERIA NA KANUNI ZAKE

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ameogopa mi ndiyo maana huwa sisomagi na hata kununua gazeti lao la michezo wapo kishabiki zaidi

      Delete
  17. Nahisi mwandishi ni muumini wa kuvunja kanuni.....

    ReplyDelete
  18. Kabla sijasoma content nasoma jina la mwananchi kwanza nionapo jina lako salehe jembe najua hakuna la maana zaidi ya kuituhumu Yanga sababu ulivamia kazi huna weledi na kazi hii aliekosoma nakala yote kama nmekosea aniambie

    ReplyDelete
  19. Naona watu wanalaumu sana Yanga kwa kukubali kucheza mechi za Azam na biashara ambazo pia Musa wake ulisogezwa mbele. Wanajenga hoja hii ni lazima pia watuambie na muda ambao taarifa ya kusogezwa mbele kwa mechi hizo ilitolewa kwa vilabi husika. La pili nashauri kila mmoja ajitahidi kuguata sheria na kanuni zilizowekwa mahali popote, iwe kazini, barabarani au mahali pengine. Kanuni zilizowekwa zikifuatwa zitaondoa migongano kama hii isiyobya lazima

    ReplyDelete
  20. Global michezo mmechemsha point yenu ni pumba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic