BADO Mei 8 itabaki kwenye kumbukumbu ya mashabiki na wadau wa mpira baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga kuyeyuka kutokana na Yanga kugomea mabadiliko ya muda.
Mchezo huo
awali ulipangwa kuchezwa saa 11:00 jioni ila siku ya mchezo, Shirikisho la Soka
Tanzania, (TFF) lilitoa taarifa kwamba muda wa mchezo utakuwa ni saa 1:00
usiku, kwa kile ilichoeleza kuwa ni kupewa maelekezo kutoka kwenye wizara.
Pia
walieleza kuwa wametoa taarifa kwa timu zote mbili ambapo Yanga walieleza kuwa
mabadiliko hayo ni kinyume cha kanuni ya 15, (10) za Ligi Kuu inayohusu taratibu za mchezo ambayo inasema:”Mabadiliko
yoyote ya muda wa kuanza mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pande zote husika za
mchezo angalau saa 24 kabla ya muda wa awali,”.
Kutokana na
tamko hilo Yanga iligomea mechi na kufanya mchezo huo kuyeyuka mazima ambapo
kwa sasa taarifa kutoka Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) imeeleza kuwa Kamati ya
Masaa 72 itakaa ili kujadili suala hilo na kutoa ratiba ya siku ya mcheo huo hizi hapa ni baadhi ya hasara ambazo
zimetokana na kuyeyuka kwa dabi hiyo:-
Muda
Maumivu
makubwa kwa mashabiki pamoja na wachezaji kutumia muda mwingi kwa ajili ya
maandalizi na mwisho wa siku hakuna ambacho wamekishuhudia.
Yupo shabiki
wa Yanga ambaye ni mwanariadha Mang’suli Hussein mwenye umri wa miaka 45 yeye
alianza safari ya kutoka Kigoma kuanzia Aprili 15 na alifika Bongo Mei 8 siku
ya mechi. Ikumbukwe kwamba jamaa aliripoti kwamba kutokana na safari hiyo
aliweza kuumwa tumbo baada ya kupima aligundulika na Typhod.
Jamaa katua
Bongo na juhudi zote ila kaambulia patupu tena alikuja kwa mguu. Hasara kubwa
kwa muda wake pamoja na nguvu.
Viporo
Simba ambao
ni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wanaongeza idadi ya
viporo kwenye mechi zao. Jumla wamecheza mechi 25 watani zao Yanga wamecheza
mechi 27.
Kwa sasa ipo Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs. Ratiba ilikuwa inaonyesha kwamba Mei 11
alipaswa kucheza na Coastal Union hivyo mchezo huu utakuwa kiporo kwa sababu
anacheza na Kaizer Chiefs Mei 15.
Weka mbali
kiporo hicho pia kuna mechi dhidi ya Namungo ambayo nayo ilikuwa inashiriki
Kombe la Shirikisho na ilitinga hatua ya makundi. Hapa ni mechi zote mbili
dhidi ya Namungo ni viporo.
Kuyeyuka kwa mchezo huo Mei 8 ni kiporo kingine kwa Simba.
Nguvu kazi
Kuna nguvu
kubwa ambayo ilikuwa imetumika kwa ajili ya mchezo huo wa Mei 8 ila kuyeyuka
kwake inakuwa ni sawa na hamna kitu.
Wapo
maripota ambao walifunga safari kutoka nje ya Dar na kuweka kambi kwa muda kwa
ajili ya mchezo huo na wengine walitoka nje ya nchi kwa ajili ya mchezo wa
Simba v Yanga. Pia hata wale ambao wapo Dar walibadilisha majukumu yao kwa
ajili ya mechi, hasara kubwa.
Zikumbuke
zile ziara ambazo Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alikuwa akizifanya kwenye
vyombo vya Habari. Uwekezaji wa Azam TV kwa ajili ya mechi hiyo, dunia nzima
ilikuwa inasubiri kushuhudia burudani, ila ghafla nguvu yote imeyuka na mwisho
wa siku inakuwa ni habari nyingine.
Mkwanja ilikuwa bado
kizungumkuti
Kwa sasa
kila shabiki ambaye aliingia uwanjani anafikiria kuhusu namna gani anaweza
kurejeshewa mkwanja wake. Baada ya mchezo kuahirishwa, mashabiki walionekana
wakilalamika kuomba kurejeshewa mkwanja wao.
Hata
Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) wameeleza kuwa wameiagiza Bodi ya Ligi
Tanzania, (TPLB) kuweza kushughulikia suala hilo ambalo ni gumzo kwa sasa.
Kukosekana kwa burudani
Mashabiki
wengi walitarajia kuweza kuona udambwiudambiwi wa wachezaji wao nyota ambao ni
pamoja na Clatous Chama, Luis Miquissone, Bernard Morrison kwa Simba na kwa
upande wa Yanga walitarajia kuona ufundi wa Saido Ntibanzokiza, Tuisila
Kisinda, Yacouba Songne ila mwisho wa siku wameambulia patupu, hasara kwao
pia.
Umebaki ni wimbo wa kila siku achamaisha mengine yaendelee kama nipesa tumeisha pigwa tusubiri majaliwa tu
ReplyDeleteYote hayo sababu ya utopolo kumuogopa mnyama
ReplyDeleteHalafu mbona kila picha yako unapenda kuonyesha Simba wakishambulia wakati mechi hiyo hawakuwa hata na short on target zaidi ya Ile Corner ya Goli?
ReplyDeleteHizo picha za kushambulia zinatoka wapi?Mlipata goli la penalti isiyo penalti. Bado tumewazidi pointi 4 na viporo 2.Mngekuwa timu ya msingekutwa baada ya kuongoza kwa pointi 9.Mmeanza kulalama kuhusu viporo mbona hamlalamiki kuhusu Namungo?Kila timu ishinde mechi zake hamna namna.
ReplyDelete