LEO Mei 19 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo kuna mechi mbili zinachezwa ili kusaka pointi tatu muhimu.
Mchezo wa mapema kabisa ni ule utakaowakutanisha Gwambina FC dhidi ya Namungo ambao unapigwa Uwanja wa Gwambina Complex.
Tayari Gwambina wameanza kusaka pointi tatu kama ilivyo Namungo, ambapo mchezo huo umeanza majira ya saa 8:00, Mwanza.
Pia mchezo huo wa Gwambina FC dhidi ya Namungo upo mubashara Azam TV ukikamilika huo unafuata ule wa JKT Tanzania dhidi ya Yanga.
Mchezo huo utachezwa saa 10:00 jioni na ni Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
0 COMMENTS:
Post a Comment