May 5, 2021


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kuna wahuni ambao wanasambaza clip ambazo zinataja viingilio vya mchezo huo kuwa ni 5,000 jambo ambalo sio kweli na lilisababisha apigiwe simu na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi Tanzania.

Manara amesema kuwa wahuni hao wamempoza kwa kuwa wamekuwa wakiisambaza clip hiyo ambayo imekuwa ikileta mkanganyiko mkubwa.

Simba ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 8, Uwanja wa Mkapa.

Manara amesema:-"Jana na juzi kuna clip inatembea sijui inataja viingilio kwamba viingilio ni 3,000, sijui 5,000 nikapigiwa simu na watu wa Bodi ya Ligi, TFF wakiniambia kwamba vile sio viingilio.

"Ile clip ni ya mwezi wa tisa kuelekea kwenye mechi yetu dhidi ya Gwambina sasa kwa kuwa iliangukia Jumamosi basi wahuni wakaamua kuitumia.

"Viingilio ni 7,000 mzunguko, 15,000 VIP C, 20,000 VIP B, 30,000 VIP A. Hakuna viingilio vya elfu tatu sijui hii ni mechi kubwa," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic