May 6, 2021

 


KIKOSI cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco jana Mei 5 kiliyeyusha pointi tatu mbele ya JKT Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed, 'Bares'.

Ushindi huo unakuwa ni sawa na kisasi kwa sababu JKT Tanzania ilipowafuata Namungo FC, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Mei 2 ubao ulisoma Namungo FC 3-2 JKT Tanzania.

Kwenye mchezo huo wa hatua ya 16 bora wa Kombe la Shirikisho, Namungo ilitinga hatua ya robo fainali na ilishuhudia mshambuliaji wao Relliants Lusajo akisepa na mpira wake baada ya kufunga hat trick.

Kwenye mchezo wa jana ambao ulikuwa ni wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Daniel Mecha alimtungua Jonathan Nahimana kwa kichwa dakika ya 5 akiwa ndani ya 18 na kuwafanya Namungo wasiwe na la kufanya kwa kuwa waliziacha pointi tatu mazima.

Ushindi huo kwa JKT Tanzania unawafanya wafikishe jumla ya pointi 30, ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo na Namungo FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 11 ina pointi 31 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.

JKT Tanzania imecheza jumla ya mechi 28 ipo kwenye hatari ya kushuka daraja kwa kuwa nafasi ambayo ipo ni nafasi ya kuweza kucheza play offs hivyo ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mechi zake ambazo zimebaki.

Bares amesema:"Kwanza tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa matokeo ambayo tumeyapata na ninawapongeza vijana wangu kwa matokeo ambayo tumeyapata.

"Tuliwasoma wapinzani wetu kwenye mchezo wetu uliopita na mwisho wa siku tumepata pointi tatu,".

Morocco amesema kuwa:"Nafasi ambayo tupo kwa sasa sio nzuri, ila bado hatujapata muda kwa ajili ya kuangalia mpango kazi lakini bado tuna kazi ya kufanya tena kwa sasa.

"Tunatakiwa turudi haraka kwenye game, ila huwezi kuhesabu mechi ambazo hujacheza ila nafikiri tuna kazi ya kubadilika kwa ajili ya mechi zinazofuata,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic