May 22, 2021


 IKIWA leo Simba inatupa karata yake ya pili mbele ya Kaizer Chiefs kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali ya pili, nyota wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein, ‘Mmachinga’ amesema kuwa Kocha Mkuu, Didier Gomes atumie viungo wengi kupata ushindi.

Mmachinga ambaye kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa Yanga Princess ambayo imemaliza Ligi ya Wanawake ikiwa nafasi ya pili amesema kuwa lazima Simba waongeze juhudi na nidhamu kwa wapinzani wao.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa FNB, ubao ulisoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba jambo linaongeza mzigo kwa kikosi cha Simba kupindua meza kwa kushinda mabao 5-0 ili kutinga hatua ya nusu fainali.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mmachinga alisema kuwa jambo la kwanza ambalo Simba inatakiwa ni kuwaheshimu wapinzani wao ikiwa watashindwa kufanya hivyo yatajirudia ya Afrika Kusini.

“Simba wanapaswa wawaheshimu wapinzani wao kwa sababu ni timu kubwa na haina presha kwenye mchezo kutokana na faida ya mabao manne waliyopata. Wacheze kwa nidhamu kubwa, wakicheza kama kule ugenini watashindwa kutimiza lengo lao.

“Kazi kubwa ya mashambulizi iwe kipindi cha kwanza wapate mabao wakishindwa hapo kipindi cha pili wataadhibiwa wao. Mfumo mzuri nadhani uwe wa kutumia viungo wengi kama watano na  washambuliaji wawili ambao ni Chris Mugalu na John Bocco,” alisema Mmachinga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic