HAMNA namna leo Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Yanga lazima kitaumana kutokana na timu zote mbili kuhitaji pointi tatu.
Novemba 7 Mwamuzi alikuwa ni Abdalah Mwinyimkuu ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba na Mei 8 mwamuzi atakuwa ni Emannuel Mwandembwa.
Kwa mujibu wa rekodi za watani hawa wa jadi katika misimu 12 mfululizo wamekutana mara 23 yamefungwa mabao 50. Simba imefunga mabao 26, Yanga imefunga mabao 24 ndani ya uwanja kwenye Dar Dabi.
Simba ilishinda mara 7, sare 10 na ushindi kwa Yanga ni mara sita twende sawa namna hii:-
Mzunguko wa kwanza ngoma ni nzito
Tangu msimu wa 2009/10-2020/21. Yanga wameshinda mara tatu katika mechi za mzunguko wa kwanza wakiwa ni vinara huku Simba ikishinda mara moja msimu wa 2009/10.
Hapa Yanga walisepa na pointi tatu ilikuwa msimu wa 2010/11, 2011/12 na 2015/16.
Mwendo wa mojamoja
Katika mechi zao nane za mzunguko wa kwanza ngoma ilikuwa ni kugawana pointi mojamoja ilikuwa 2012/13, 2013/14, 2014/15, 2016/17, 2017/18, 2018/19, 2019/20, 2020/21.
Mzunguko wa pili kwa Mkapa kitaumana
Leo kitaumana kwa kuwa katika mechi 11 walizokutana mzunguko wa pili rekodi zinaonyesha kwamba Simba wamekuwa wakisepa na pointi tatu.
Dakika 90 zitaamua, ajabu ni kwamba kwenye mechi hizo sita za ushindi zote Yanga walikuwa ni wenyeji wa mchezo.
Watani zao wa jadi Yanga walishinda kwenye mechi tatu na sare mbili.
Ushindi wa Simba
Za mzunguko wa pili Simba ilishinda msimu wa 2009/10, 2011/12, 2014/15, 2016/17, 2017/18 na 2018/19.
Ushindi wa Yanga
Yanga imeshinda mechi tatu 2012/13, 2015/16 na 2019/20 .
Ngoma droo
Sare zilipatikana mbili mzunguko wa pili ilikuwa ni msimu wa 2010/11 na 2013/14.
Sura mpya
Novemba 7, wakati Michael Sarpong wa Yanga na Joash Onyango wa Simba wakizifungia timu zao kwenye sare ya kufungana bao 1-1, kwenye benchi la Yanga, Kocha Mkuu alikuwa ni Cedric Kaze na kwa upande wa Simba alikuwa ni Sven Vandenbroeck.
Kwa sasa sura hizo zote zimeshasepa Bongo, Kaze alifutwa kazi kwa kile kilichoelezwa ni matokeo mabovu kwa mzunguko wa pili na Sven yeye alibwaga manyanga baada ya kupata dili Moroco.
Ni Didier Gomes yeye yupo Simba kwa sasa akiwa ni kocha mkuu na alisema kuwa anahitaji pointi tatu kwenye mchezo wake dhidi ya Yanga.
Na Nassredine Nabi, yupo ndani ya timu ya Yanga ambapo alisema kuwa anahitaji kuona vijana wake wakifanya kazi kwa vitendo kwenye mechi zote ikiwa ni pamoja na ya kesho dhidi ya Simba.
Rekodi zao hizi hapa:-
2009/2010
Oktoba 31, 2009, Simba 1-0 Yanga, Aprili 18, 2010 Simba 4-3 Yanga.
2010/2011
Oktoba 16, 2010, Yanga 1-0 Simba, Machi 5, 2011, Simba 1-1 Yanga.
2011-12
Oktoba 29, 2011, Yanga 1-0 Simba, Mei 6, 2012,
Simba 5-0 Yanga.
2013/14
Oktoba 20, 2013, Yanga 3-3 Simba, Aprili 19, 2014 Simba 1-1 Yanga.
2014/15
Oktoba 18, 2014, Simba 0-0 Yanga, Machi 8/2015
Simba 1-0 Yanga.
2015/16
Septemba 26, 2015, Yanga 2-0 Simba, Februari 20, 2016, Yanga 2-0 Simba.
2016/17
Oktoba Mosi, 2016, Simba 1-1 Yanga, Februari 26, Simba 2-1 Yanga.
2017/18
Oktoba 28, Yanga 1-1 Simba, Aprili 29, Simba 1-0.
2018/19
Septemba 30, Simba 0-0 Yanga, Februari 16, Yanga 0-1 Simba.
2019/20
Januari 4, 2020 Simba 2-2 Yanga, Machi 8, Yanga 1-0 Simba.
2020/21
Novemba 7, Yanga 1-1 Simba, Mei 8, Simba v Yanga?
Nafasi zao
Simba kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ina pointi 61 baada ya kucheza mechi 25, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza jumla ya mechi 27.
0 COMMENTS:
Post a Comment