UONGOZI wa Arusha FC umeweka wazi kwamba unawaheshimu wapinzani wao Ndanda FC ila utaingia kwa hesabu za kupata ushindi ili kubaki ndani ya Ligi Daraja la Kwanza.
Mchezo wa leo ni playoff ya kusaka kubaki ndani ya Ligi Daraja la Kwanza na yule ambaye atapoteza katika matokeo ya jumla atashuka mpaka Ligi Daraja la Pili.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Arusha FC, Yasinta Amos amesema kuwa wachezaji wapo vizuri kwa ajili ya mchezo wao wa leo dhidi ya Ndanda FC.
“Maandalizi yapo vizuri na kwa mujibu wa ripoti inaonyeshwa kwamba hakuna majeruhi hivyo kikosi kipo imara na ari ni kubwa kwa vijana. Tunaamini kwamba mchezo wetu utakuwa na ushindani mkubwa.
“Tunawaheshimu Ndanda ila nasi tunahitaji ushindi ili kuona kwamba tunakuwa na mwelekeo mzuri kwa kubaki ndani ya Ligi Daraja la Kwanza, tupo vizuri na tunahitaji ushindi.
"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwani kila kitu kipo sawa na tunaamini kwamba tutapata matokeo,".
Arusha itaanza kumenyana na Ndanda FC, Mei 22 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na ule wa marudio utakuwa ni Uwanja wa Nangwanda, Mei 29.
0 COMMENTS:
Post a Comment