NYOTA wawili wa Yanga wamekumbwa na hali ya kufanana kwa kuondolewa kwenye kikosi kwa kosa la utovu wa ndhamu.
Leo Mei 25, Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mwadui FC huku ikitarajiwa kuwakosa nyota wawili ambao wamesimamishwa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.
Mchezaji wa kwanza kusimamishwa kwa kosa la utovu wa nidhamu ni nahodha Lamine Moro ambaye alisimamishwa wakati timu ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa Moro alisimamishwa kutokana na Nabi kueleza kwamba alikuwa na makosa ya kinidhamu.
Nyota mwingine ambaye ametajwa kuwa amesimamishwa na Nabi kutokana na utovu wa nidhamu ni kipa namba moja Metacha Mnata.
Mnata anatajwa kusimamishwa na Nabi kwa kosa la utovu wa nidhamu hivyo naye huenda ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Mwadui FC.
Mnata ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo aliibuka hapo akitokea Klabu ya Mbao ambayo kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza lakini msimu ujao itashiriki Ligi Daraja la Pili kwa sababu imeshuka pia daraja.
Anayefuata kusimamishwa ni kocha mwenyewe
ReplyDeleteBaada ya Simba kutolewa CAF Sasa mnaendelea ku demorize isiwe na Harmon ili Timu lenu Thimba lipate mteremko ,mlimtumia Lamine kututengenezea Date zile,Leo mnaanza maana Sasa kila la Yanga unaloandika ni negative Akhasante Friend of Simba
ReplyDeleteSafi sana endeleeni kuamini hivyo hivyo mpaka mtakapo amka tutakuwa tumewaacha mbali sana
DeleteYaani Simba ndio wamewatuma Metacha na Lamine wakose nidhamu.Wakati mwingine inabidi tuache visingizio vya kitoto na tuwajibike.Pia Simba wamemtuma Nabi kocha wa Yanga awaadhibu hao wachezaji kwa ukosefu wa nidhamu. Inabidi Yanga tujiangalie kwenye kioo tabia ya kutafuta kisingizio kwenye kila jambo ni ujinga mtupu Tubadilike.
ReplyDeleteTimu isiyo na utulivu isitaraji kitu. Huyo kipa aliesimamishwa kwa kukosa nidham inasemekana yupo mbioni kutimka na kuelekea kuleeeee
ReplyDeletewww.sokaleo.com
ReplyDelete