May 25, 2021


 
CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wanatakiwa kuripoti kambini leo kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao za Ligi Kuu Bara.

KMC ilitoa mapumziko kwa wachezaji wake kuanzia Mei 17 mpaka Mei 25 baada ya timu hiyo kutokuwa na mchezo wowote wa mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kwa muda wa mwezi mmoja.

 Akizungumza na Saleh Jembe Mwagala amesema kuwa wachezaji wanarejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao.

“Tulitoa mapumziko kwa wachezaji na tuliwaambia kwamba Mei 25 wanapaswa kurudi kambini. Kwa hiyo leo wanapaswa kurudi kambini na Jumatano tutaanza mazoezi mepesi.

“Hii itakuwa maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji ambao unatarajiwa kuchezwa Mei 17, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma,”.

Kwenye msimamo wa ligi, KMC ipo nafasi ya 5 baada ya kucheza mechi 29 itakutana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 8 na pointi zao ni 39 baada ya kucheza mechi 30.

Huo utakuwa ni mchezo wa pili ambapo walipokutana mzunguko wa kwanza Uwanja wa Uhuru, Desemba 4, ubao ulisoma KMC 1-0 Dodoma Jiji.

2 COMMENTS:

  1. Hawa huwa mnawatangaza lkn hawafiki popote wasipoachana na Usimba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kila Kona Simba, Simba, Simba, Simba.... Sasa nimeamini MNYAMA ANATISHA

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic