May 23, 2021


 BAADA ya awali mchezo wa Ligi Kuu Bara kupangwa kuchezwa Mei 8, Uwanja wa Mkapa na waamuzi kupatikana  sasa imekuwa ni pasua kichwa kujua nani atakuwa mwamuzi watakapokutana Julai 3.

Awali kabla ya mchezo huo kuota mbawa, waamuzi ambao walipangwa ilikuwa ni pamoja na Emmanuel Mwandembwa aliyepewa jukumu la kuwa mwamuzi wa kati, Frank Komba aliyepangwa kuwa mwamuzi msaidizi namba moja, Hamdani Saidi aliyepangwa kuwa mwamuzi namba mbili pamoja na Ramadhan Kayoko ambaye alipangwa kuwa mwamuzi wa akiba.

Baada ya mchezo huo kuyeyuka kutokana na Yanga kugomea mabadiliko ya muda kwa kueleza kuwa mabadiliko ya muda uliofanywa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kutoka saa 11:00 jioni mpaka saa 1:00 usiku ni kinyume cha utaratibu wa kanuni. Jambo hilo lilifanya mchezo huo ughairishwe kwa kuwa timu zilitofautiana muda wa kwenda.

Yanga walipeleka timu uwanjani saa 10:20 na ilisepa saa 11:40 jioni na Simba ilipeleka timu saa 11:25 jioni jambo lililofanya ngoma isichezwe na kwa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania mchezo huo utachezwa saa 11:00 jioni, Julai 3.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania, Sud Abdi Mohamed amesema kuwa kwa sasa ni mapema kusema kama waamuzi hao watakuwepo kwenye mchezo ujao.

"Ni mapema kusema kama watabaki hao kwenye mchezo ujao maana lolote linaweza kutokea,". 


10 COMMENTS:

  1. Mechi mwezi wa saba, hata june bado unawatafuta wa nini leo? Au ndio maandalizi yale, maana wale wa awali walishakula advance. Hawapangwi tena hao. Safari hii wanatoka ethiopia ha ha ha

    ReplyDelete
  2. Tff fc kazi wanayo ya kupanga matokeo

    ReplyDelete
  3. Tff fc kazi wanayo ya kupanga matokeo

    ReplyDelete
  4. Ukweli ni kwamba waamuzi wengi ni Simba Sasa hawataki Waamuzi ambao ni Bora basi Kama hawataki Wachache walio wakweli tuingie gharama watoke nje na siyo Rwanda au Burundi au Kenya nk ni Ulaya walipwe cse Simba na Mo na KARIA wanawaonga inajulikana tuache porojo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Safari hii hamuoni kipengere cha kanuni kitakacho halalisha kukimbia ndo maana mnataka kusingizia waamuzi... Safari hii mkikimbia tunawafuata kokote mtakakoenda lazima game ichezwe

      Delete
  5. Jana tu dk 5 kila kipindi inachekesha sanaa

    ReplyDelete
  6. Mbona sisi Wananchi game kama hizi tunaletewaga Waarabu (waaamuzi) au watu wa mbali mi nahoji uadirifu wa CAF inatia Giza kuongea kataa kubali.

    ReplyDelete
  7. Kwa mawazo hayo utopolo mtasubir mtasubir sana kupiga hatua

    ReplyDelete
  8. Kwan uliona refa kapendelea Simba? Ile penati ya mtu kushika ndani ya box ingekuwa Utopolo sa hizi washafika FIFA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic