Na Saleh Ally
JIBU
la mechi ya watani Yanga na Simba halipatikana hadi Jumamosi Mei 8, yote sasa
yanayozungumzwa ni stori kama sehemu ya utangulizi.
Mechi inakuja lakini kuna wachezaji ambao wanaweza kuimaliza mechi hiyo nje ya mifumo ya makocha kwa maana ya uwezo wao binafsi. Wanaweza kuwa wengi katika kila timu, lakini baadhi ya nitakaowataja wanaweza kuwa hatari kutoka kwa kila upande.
Uwezo binafsi, kipaji, uzoefu vinaweza kuwa sehemu ya vigezo vya kuwafanya wao kuwa bora na kuzibeba timu zao kupata matokeo ambayo yalikuwa hayajatarajiwa.
Yacouba:
Amekuwa
na mwendo mzuri sana na unamuona aina yake ya uchezaji ni yule anayeweza kuwa
msaada mkubwa katika kikosi chake nje ya mfumo. Ana uwezo wa kukimbia na mpira
na kuwatambuka hata mabeki wawili au watatu.
Uwezo
wake ni kutoa pasi za mabao au kufunga lakini ana uwezo wa kutengeneza nafasi
au kuanzisha mashambulizi. Huyu atakuwa hatari kwa ngome ya Simba na lazima
wawe makini naye.
Tuisila:
Mechi
ya mzunguko wa kwanza alikuwa mfano, alifanya anachotaka na kusababisha penalti
kwa kazi ya uwezo wake binafsi. Inawezekana akafanya hivyo wakati huu kwa kuwa
anajua mechi hii ni kubwa hivyo lazima atataka afanye jambo la kukumbukwa.
Kisinda anaweza kuwa sehemu tishio la mfumo wa ushambulizi wa Simba kutokana na kasi yake. Maana yake Zimbwe Jr, atalazimika kutopanda muda mwingi ili asirudie kama kosa la mechi ya mzunguko wa kwanza, kosa ambalo mwisho Onyango akienda kujaribu kurekebisha, akajikuta akifanya makosa.
Uwezo wa Kisinda kama mchezaji
mmoja anayeweza kubadili matokeo ni mkubwa sana.
Ntibazonkiza:
Saido
Ntibanzokiza ni mmoja wa wachezaji wakubwa, wenye uzoefu mkubwa wanaocheza Ligi
Kuu Bara. Mechi ya Simba ni kubwa lakini kwa uzoefu wake, haiwezi kumsumbua kwa
maana ya presha, labda kama ataipania sana, inawezekana kukawa na ugumu kwake.
Aina
ya uchezaji wake, anaweza kuwa nje ya mfumo na bado akafanya vizuri zaidi
kutokana na uwezo. Angalia advantage ya mipira iliyokufa. Angalia utoaji asisti
au utengenezaji nafasi lakini shooting yake ni ya kiwango cha juu kwa maana ya
target. Huyu ni moja ya mwiba wanaoweza kuutumia Yanga kuiadhibu Simba.
Carlinhos:
Mtaalamu
ambaye anaweza kusababisha mabao kwa asisti au kutengeneza au kuanzisha
mashambulizi. Upigaji wa mipira ya faulo ni hatari lakini Simba lazima wawe
makini kufanya faulo nyingi karibu na lango lao kwa kuwa kwa Muangola huyu, ni
rahisi kufunga kama ilivyo kwa Saido.
Wachezaji
wa aina yake, huonekana katika mechi kubwa kama hiyo ya Simba kwa kuwa inatoa
nafasi ya kucheza tofauti na zile mechi zinazotumia nguvu zaidi.
Miquissone:
Kwa
upande wa Simba, bila shaka Luis anakuwa hatari kwa karibu kila timu
anayokutana nayo. Kwa Yanga amekuwa hatari lakini bado hajasababisha madhara
makubwa, jambo ambalo bila shaka hata yeye atataka kulifanya kudhihirisha ubora
na ukubwa wake.
Kasi
yake, uwezo wake wa kutoa pasi za mabao na kutengeneza nafasi lakini uwezo
mkubwa wa kushuti na kulenga lango ni mwiba kwa mabeki wa Yanga. Pia wanaotumia
nguvu sana wanapaswa kujichunga kwa kuwa anaweza kuwasababishia kadi hata
nyekundu na kuifanya timu yao kucheza pungufu.
Morrison:
Akiingia
sasa anaonekana ni hatari zaidi ingawa Gomes ndiye atakuwa mwamuzi wa mwisho,
kwamba iwe surprise start au aingie kama super sub. Lakini ameimarika na
anaonekana yuko katika kile kiwango walichokuwa wanakitaka Simba. Anafunga,
anatoa asisti lakini ana akili ya haraka kuiendesha timu katika sehemu ambayo
ilionekana imechelewa kwa maana ya spidi.
Mugalu:
Wako
waliosema anakosa sana mabao, lakini kama Gomes ataanza naye. Ana uwezo wa
kuwatuliza Shaibu Ninja na Dickson Job kama wataanza wasiende popote na mwisho
kuwapa nafasi viungo wao kuwa na nafasi kubwa ya kutamba. Ana nguvu sana na
anaweza kuwa sehemu ya kuifanya Yanga kugawanyika kwa kuwa mabeki wa kati
watalazimika kucheza chini. Ingawa amekosa nafasi nyingi, lakini bado ana
nafasi kubwa ya kumalizia na kubadili matokeo.
Kagere/Bocco:
Hawa
wawili ni hatari sana kwa Yanga kutokana uzoefu wao na mechi ya watani,
wakipata nafasi ya kucheza lazima Yanga wawe makini nao sababu ya mipira ya
vichwa lakini utulivu wao wa Kariakoo Dabi kwa kuwa wanaijua faida na maana
yake lakini wana uwezo wa kuibadilisha na kuifanya Simba ishinde.
Kiuwezo
wanao lakini wamekosa nafasi nyingi, lakini uzoefu unaweza kuwa chachu kubwa ya
wao kuwa hatari kwa Yanga.
Kama kwa upande wa simba hujamweka Chama, basi labda sielewi lengo lako. Huyu ndio mpango mzima kwa uchezaji wa simba
ReplyDeleteKatika wachezaj wote aliowataja inamaana chama kiwango chake n kdogo,,,huyu mwandishi chiz kwel
ReplyDeleteTangu lini akachambua mpira unaoeleweka huyu???
ReplyDelete