BAADA ya kusepa na pointi tatu muhimu mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Yanga wameweka wazi kwamba hesabu zao kubwa ni kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mwadui FC.
Mei 19, ubao wa Jamhuri, Dodoma baada ya dakika 90 ulisoma JKT Tanzania 0-2 Yanga ambapo watupiaji walikuwa ni Yacouba Songne na Tuisila Kisinda.
Yanga ilitinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambalo bingwa wake mtetezi ni Simba baada ya ubao wa Uwanja wa Nelson Mandela kusoma Prisons 0-1 Yanga na mtupiaji alikuwa ni Yacouba Songne.
Injinia Hersi Said ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Usajili ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa wanahitaji kwenda kupata ushindi mbele ya Mwadui FC ili kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho.
“Tukimaliza kazi mbele ya JKT Tanzania, safari yetu itakuwa ni kwenda Shinyanga ambapo huko tunakwenda kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mwadui FC, bado malengo yetu ni kufanya vizuri na nafasi ipo kwa sababu wachezaji wapo tayari,”.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kamabarage Mei 25 na mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Biashara United ama Namungo katika hatua ya nusu fainali.
Tayari kazi na JKT Tanzania wameshamaliza na kwa sasa Yanga imeshatia timu Singida kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa sababu wadui haina cha kupoteza.
Wakimaliza kambi kwa muda Singida wataelekea Shinyanga kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mwisho.
Ikumbukwe kuwa walipokutana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Kambarage, ubao ulisoma Mwadui 0-5 Yanga.
Manyani bhana mtimu wenyewe hovyo eti wanataka kombe
ReplyDeleteMkiitana manyani wenyewe mwisho wa siku mnaitwa manyani nna wageni mnawafukuza... hivi watu weusi wamelaanika au tunajilaani wenyewe?
DeleteKama imekuuma chomoa... Mnavyowashabikia wageni ndo mnaona sawa
Delete