MTAMBO wa mabao ndani ya Ligi Kuu Bara Prince Dube amerejea uwanjani baada ya kukosekana katika mchezo uliopita dhidi ya Gwambina FC.
Dube ambaye ni namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao 14 na pasi tatu za mabao alikuwa anasumbuliwa na majeraha jambo lililofanya awakose Gwambina FC.
Licha ya kwamba hakuwa katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina bado ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 4-1 Gwambina FC.
Kwa sasa kikosi cha Azam FC kinajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa, Lindi.
Katika mchezo wa raundi ya kwanza Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Azam FC 2-2 Namungo FC hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment