NYOTA wa Simba, Bernard Morrison ameomba kukutana na shabiki wa timu hiyo Michael Filbert ambaye ametembea kwa miguu kutoka Kigoma mpaka Dar es Salaam.
Sababu kubwa ya shabiki huyo kufanya hivyo ni kwa ajili ya kushuhudia mchezo wao dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa.
Juni 21 Michael aliwasili Dar baada ya kutumia siku 15 na alipokelewa na mashabiki wa Simba na kundi la Simba Ushirikiano kutoka Kigogo.
Kupitia Ukurasa wa Instagram wa Mwandishi wa EATV, Zainabu Rajabu baada ya kuposti habari ya shabiki huyo kutua Bongo, Morrison aliandika:"Nahitaji kumuona yeye katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo wa leo tafadhali,".
Leo Juni 22, Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya City.
Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku.
Safi sana
ReplyDeleteWapenzi wa Simba hawaipendi timu yao kinafiki lakini kwa roho zao zote
ReplyDeleteHongera sana Michael kutoka Kigoma hadi Dar es Salaam kwa Mguu ni Safari ndefu sana.
ReplyDeleteMafii kabisa
ReplyDeleteAliona mwingine kapandishwa ndege......watakuja wengi
ReplyDeleteHahahahaaaaaaaaa
DeleteHaiingi akilini mtu atembee kutoka Kigoma hadi Dar kwa siku 15!!!! awe mkweli tu kuwa alikuwa anadandia vipando
ReplyDeleteDistance from Kigoma to Dar is 1,370kms. 1,370 divide by 15, is 91.333. Hivyo hiyo jamaa alikuwa anatembea 91kms kwa siku, ambao ni umbali sawa na kutoka city centre, Mnara wa saa mpaka Chalinze, pale kona barabara ya Morogoro na Tanga zinaachana...Duh,hilo ni changa la moto.
ReplyDelete