VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kupata pointi moja mbele ya Namungo kwao imetokana na mbinu za wapinzani wao kuwa sawa.
Jana, Juni 21 Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 0-0 Azam FC na kuwafanya wasepe na pointi moja.
Bahati amesema:"Namungo ni timu nzuri na kila timu kwenye mchezo ilikuwa inahitaji ushindi na mwisho wa siku hakuna ambaye ameshinda.
"Mbinu ya Namungo ilikuwa ni sawa na kwetu na kwa kuwa tumepata pointi moja kwetu ni nzuri na ilikuwa ili ushinde ilikuwa unahitaji kushinda kwa kutumia mipira ya kutengwa.
"Bahati mbaya sana kwetu Namungo waligundua hilo na mwisho wa siku hatukuweza kupata faulo hizo na tukaambulia pointi moja," amesema.
Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 32 na ina pointi 64 huku Namungo FC ikiwa nafasi ya 5 na pointi 43.
0 COMMENTS:
Post a Comment