JOHN Bocco, nahodha wa Simba ambaye ni mzawa ameweka rekodi yake kwa kuzitungua timu mbili nje ndani akimuweka kando kimtindo mshikaji wake Prince Dube wa Azam FC ambaye ameitungua timu moja pekee.
Wote wawili kwa sasa ni namba moja kwa utupiaji ambapo wana mabao 14, anayewafuata ni Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 11 ila hajaweza kuweka rekodi ya kufunga timu moja mara mbili.
Desemba 13, Uwanja wa Sokoine dk 33 Bocco alifunga bao pekee la ushindi lililoipa pointi tatu mazima Simba alirudia tena walipokutana Uwanja wa Mkapa, Juni 22 ambapo alifunga bao lake la 14 ilikuwa ni dk ya 47.
Mbali na Mbeya City, timu nyingine ambayo alifunga nje ndani ilikuwa mbele ya Mwadui FC aliwatungua Oktoba 31 mabao mawili dakika ya 25 na 64 kwa guu lake la kulia na dakika ya 66 aliwatungua kwa kichwa Uwanja wa Kambarage, Aprili 18.
Kwa upande wa Dube yeye aliwatungua Kagera Sugar ilikuwa Oktoba 4, dakika ya 5 kwa guu la kulia na dakika ya 88 kwa guu la kushoto ilikuwa Uwanja wa Azam Complex. Mara ya pili mbele ya Kagera Sugar ilikuwa Machi 3, Uwanja wa Kaitaba dakika ya 26 aliwatugua bao moja kwa guu la kulia.
0 COMMENTS:
Post a Comment