WAKATI ikielezwa kwamba Yanga inawavizia Meddie Kagere na Jonas Mkude waachwe na Simba ili wawasajili, habari mbaya kwao ni kwamba, nyota hao kila mmoja aliongeza mkataba wa miaka miwili.
Mbali na nyota hao, pia kipa aliyekosa nafasi kubwa ya kucheza kikosini hapo, Beno Kakolanya, naye ameongeza miaka mingine miwili kuendelea kuwa ndani ya Simba na kufanya jumla ya nyota watatu wenye uhakika wa kuwa ndani ya kikosi hicho msimu ujao.
Nyota hao walikuwepo sehemu ya wachezaji ambao mikataba yao ilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini kutokana na umuhimu wao, wameongezewa.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, tangu miezi miwili iliyopita, Simba imemalizana na Mkude na Kagere baada ya kuwasainisha kwa siri.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, mabosi wa Simba wamewasainisha nyota hao mikataba baada ya kupata taarifa za kuwindwa na Yanga.
“Tulikuwa tunawaangalia Yanga wakiendelea kupiga kelele za kuhitaji saini za wachezaji wetu Kagere na Mkude, nikuhakikishie kuwa, wachezaji hao walisaini mikataba miezi miwili iliyopita.
“Kama Simba ingekuwa haijamuongezea mkataba Mkude isingepata tabu ya kuhangaika naye mara kumpeleka hospitali kumpima na badala yake tungeachana naye. Ukweli ni kwamba Mkude na Kagere bado wataendelea kuichezea Simba hadi 2024.
“Kakolanya yeye alisaini mkataba Jumatatu usiku, ni baada ya benchi la ufundi kupendekeza aongezewe mkataba wa miaka miwili,” alisema mtoa taarifa huyo.
Simba kupitia kocha wake mkuu, Mfaransa, Didier Gomes, hivi karibuni alisema: “Wachezaji wote nitakaowahitaji hawataondoka Simba na badala yake nitawaongezea mikataba.
“Ninafurahia kufanya kazi na wachezaji wangu muhimu ambao wameipambania timu katika Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo nisingetamani kuona wanaondoka na badala yake waendelee kubakia hapa," .
Hizo ni kelele za mawakala aka udalali ili itoke hela ndefu wapate commission kubwa. Yanga hawahusiki na chochote.
ReplyDelete🚶🚶🚶
ReplyDeleteUtopolo bado, laleni mkue
ReplyDelete