June 23, 2021


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union ya Tanga amesema kuwa makosa ambayo wanafanya wachezaji wake yeye anapaswa kupewa lawama.

Jana Juni 22 ikiwa Uwanja wa Neslon Mandela baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tanzania Prisons 2-2 Coastal Union.

 Mchezo huo ulishuhudia jumla ya mabao manne yakifungwa ambapo kwa upande wa wenyeji Tanzania Prisons ni Samson Mbangula alipachika bao dk 19 na Jeremia Juma alifunga la pili dk ya 36.

 Abdul Suleiman alipachika bao la kwanza kwa Coastal Union dk 23 na Mudhathir Said dk 85.Kugawana kwa pointi mojamoja kumewafanya Tanzania Prisons kufikisha jumla ya pointi 42 nafasi ya 7 huku Coastal Union ikiwa nafasi ya 16 na pointi 34.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa mwendo ambao wanakwenda nao haupendezi ila yeye anapaswa kupewa lawama.

"Ninasema kwamba lawama zote ambazo zinawahusu wachezaji nipewe mimi kwa sababu mimi ni mwalimu na mbinu ninawapa mimi.

"Ambacho tunakifanya ni kuchukua makosa na kuyafanyia kazi hivyo bado tutazidi kupambana mpaka pale tutakapomaliza mechi zetu," amesema.

Coastal Union imebakiwa na mechi tatu mkononi ambazo ni dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa, Mwadui Uwanja wa Mkwakwani na Kagera Sugar.

2 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Mawazo ya kijinga sana, mkiitwa mtoe ushahidi mnajinyea nyea halafu mkipewa adhabu mnasema mnaonewa.... Endeleeni na akili zenu hizo hizo mpaka 2030 mtakapozinduka mtakuta wenzenu mbali zaidi ya sasa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic