KWA mujibu wa Meneja wa Dickson Ambundo kiungo mshambuliaji anayekipiga ndani ya Dodoma Jiji, dili la mteja wake kujiunga Yanga limefikia hatua nzuri.
Ally Mohamed ambaye ni meneja ameweka wazi kwamba muda si mrefu kila kitu kitakamilika kwa nyota huyo kujiunga na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassreddine Nabi.
"Yanga tumefika nao katika hatua nzuri ya kukamilisha dili hili kwa sababu walishawasilisha ofa na tukawa tumefika sehemu nzuri.
"Kwa sasa tunasubiri kukamilisha taratibu za mwisho ili kuona namna gani dili hilo litakamilika," amesema.
Ambundo amekuwa kwenye kiwango bora ndani ya Dodoma Jiji ambapo kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes aliweka wazi kwamba ni moja ya wachezaji waliomvutia.
Nenda utopolo tu Ambundo utapata namba,,, simba utaozea benchi ndg yangu
ReplyDelete