June 22, 2021


NYOTA wa kikosi cha Al Hilal, kiungo Last Jesi imeelezwa kuwa amemalizana na mabosi wa Azam FC kwa dili la miaka miwili.

Nyota huyo inaelezwa kuwa alikuwa anapigiwa hesabu na Simba ambayo ilimuona katika mashindano ya Simba Super Cup 2021.

Taarifa kutoka mtu wa karibu wa nyota huyo imeeleza kwamba tayari ameshaanza mazoezi ndani ya Uwanja wa Azam Complex.

"Jesi ameanza mazoezi ndani ya Uwanja wa Azam Complex hivyo kama Simba ama Yanga wanamhitaji itakuwa mpaka Azam FC wenyewe waamue kumuacha," ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa zimeeleza kuwa tayari mabosi wa Azam wamempa dili la miaka miwili nyota huyo ili aweze kuwa katika kikosi chao kwa msimu wa 2021/22.

Kiungo huyo aliweka wazi kwamba yupo Dar ila kuhusu masuala ya usajili hakuwa tayari kuzungumzia.

"Ni kweli nipo Dar kwa sasa ila kuhusu hizo za Simba, Yanga ama Azam FC siwezi kuzungumzia," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic