STAA wa Real Madrid, Eden Hazard amefunguka kuwa hana uhakika kama atarudi kwenye ubora wake ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.
Nyota huyo amekuwa akiunguza majeraha kwa misimu miwili mfululizo mara baada ya kutua Madrid akitokea kikosi cha Chelsea.
Nyota huyo baada ya kujiunga na Real Madrid amekwama kutamba katika kikosi hicho akiwa ametupia mabao manne ndani ya La Liga katika misimu hiyo yote.
Hazard amesema:"Mpaka sasa sijui kama enka yangu itarudi kama ilivyokuwa zamani na sidhani kama nitakuwa kama nilivyokuwa miaka 10 iliyopita kutokana na tatizo hilo.
"Sina shaka sana na ubora wangu hasa ninapokuwa na mpira mguuni lakini majeraha yameniathiri pakubwa," .
0 COMMENTS:
Post a Comment