MANCHESTER City mabingwa wa Ligi Kuu England imeelezwa kuwa inahitaji kupata saini ya mshambuliaji wa kikosi cha Tottenham, Harry Kane ambaye anahitaji kupata changamoto mpya msimu ujao.
Mbali na City kufungua dili la kuzungumza na nyota huyo pia Manchester United na Chelsea nazo zinatajwa kuiwinda saini ya nyota huyo anayecheza ndani ya timu ya taifa ya England akiwa ni nahodha.
Dau ambalo wanatajwa kuweka mezani City ili kupata saini ya mshambuliaji huyo ni pauni milioni 100 huku Tottenham wao wakiwa hawana mpango wa kumuuza nyota huyo kwa kuwa bado wapo na mpango naye.
Kane amesema kuwa kwa sasa akili zake ni kwenye mashindano ya Euro 2020 hivyo hana maamuzi ya kufanya kuhusu ambapo atakuwa msimu ujao mpaka pale mashindano yatakapofika tamati.
Mwenyekiti wa Manchester City, Khaldoon Al Mubarak, mwezi uliopita alisema kuwa timu timu hiyo ina mpango wa kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi hicho kwa ajili ya mashindano ambayo watashiriki.
"Tunahitaji kuwa kwenye ushindani na lazima tuwe tayari katika kufanya kazi. Ubora na uimara wa kikosi kwetu ni jambo la msingi,".
0 COMMENTS:
Post a Comment