UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba utafanya usajili katika eneo la ushambuliaji ili kuongeza nguvu kwa ajili ya msimu ujao.
Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 na safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 49 ikiwa imecheza jumla ya mechi 31.
Pia safu ya ulinzi inayoongozwa na Bakari Mwamnyeto imeruhusu jumla ya mabao 21 huku ile ya Simba inayoongozwa na Joash Onyango ikiwa imeruhusu mabao 11 kati ya mechi 27.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wameona mahali ambapo kuna mapungufu hivyo watafanyia kazi kwa kusajili kwenye nafasi ya ushambuliaji na ulinzi.
“Msimu huu kuna mambo tumeyaona na kilichobaki kwa sasa ni wazi kwamba bado tunajenga timu, tutaongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji na ulinzi ili tuweze kufanya vizuri msimu ujao.
“Mashabiki waendelee kutupa sapoti wasikate tamaa tupo imara na tutafanya vizuri bila mashaka kwani kujenga timu kunahitaji muda,” amesema Nugaz.
Miongoni mwa wachezaji ambao walisajiliwa na Yanga ni pamoja na Wazir Junior mwenye mabao mawili, Michael Sarpong mwenye mabao manne, Fiston Abdulazack mwenye bao moja ndani ya ligi.
Mnahangaika kuweka tetesi za usajili zote mnakosea kwanini msiache tu na kukaa kimya mkiwa hamjui?
ReplyDeleteTutahangaika sana lakini kwanza tujipange kinidham na tuwe kitu kimoja, sio huyu anapanda na mwengine anangoa majungu yawe mwiko timu iwe na mshikamano au tutaleta nyota wa mabilioni tuondokee patupu. I Mchezaji akikosea peneti atasakamwa na kuzomewa mpaka atake kusepa mwenyewe tumewashuhudia akina Boco, Mugilu,Onyango Kagere na Chama wskikosa peneti na Manula akiruhusu magoli lakini hakuna hata mmoja aliezomewa au kuandamwa na huyo huyo Manula Leo amebaki kati ya magoli kipa bora Africa
ReplyDeleteumesahau wakati manula anasemwa na mashabiki wa simba wakisisitiza kakolanya akae golini badala ya manula ?
DeleteAfrika gani unaisema?
Delete