MENEJA wa timu ya taifa ya Tanzania, Nadir Haroub, 'Canavaro' amesema kuwa watatoa taarifa kuhusu nyota watatu ambao hawajaripoti kambini hivi karibuni.
Kwa sasa timu ya taifa ya Tanzania ipo kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Julai 13 saa 10:00 jioni.
Akizungumza na Saleh Jembe, Canavaro amesema kuwa nyota hao watatu taarifa zao zitatolewa hivi karibuni:"Kuhusu Mbwana Samatta, (anayecheza Fernabache akitokea kwa mkopo Klabu ya Aston Villa) Simon Msuva, (Wydad Casablanca ya Morocco) na Novatus Dismas( Makab Tel Aviv ya Israel) hawa bado hawajaripoti na taarifa yao itatolewa hivi karibuni.
“Kikubwa mashabiki waendelee kuipa sapoti timu yao kwani tunaamini kwamba vijana wapo tayari kwa ajili ya mapambano na tunachohitaji ni matokeo chanya,” amesema Canavaro.
0 COMMENTS:
Post a Comment