June 11, 2021


JOSE  Mourinho, amesema kuwa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kinaweza kufanya vizuri katika mashindano ya Euro 2020 ambayo yanatarajiwa kuanza leo kutokana na kuwa na kikosi kizuri kinachowajumuisha wachezaji ambao sio wabinafsi ikiwa ni pamoja na Karim Benzema.

Mourinho ambaye alimfundisha Benzema na Cristiano Ronaldo ndani ya Real Madrid ameongeza kuwa sababu nyingine ambayo iliwafanya wawili hao kuwa marafiki ni kutokana na hali ya Benzema kutokuwa mbinafsi katika kutengeneza nafasi za kufunga jambo ambalo lilikuwa linamfurahisha Ronaldo.



Kocha huyo raia wa Ureno amesema kuwa imani yake kubwa kuelekea kwenye michuano ya Euro 2020 washambuliaji ambao amefanya nao kazi kwa nyakati tofauti ikiwa ni pamoja na Ronaldo, Benzema, Harry Kane na Romelu Lukaku ni miongoni mwa washambuliaji makini na bora.

Mourinho amesema kuwa katika utendaji wake wa kazi alikuwa anashangazwa na mabao ambayo yalikuwa yanafungwa na Harry Kane. Amebainisha kuwa uwepo wa Benzema katika kikosi cha timu ya Ufaransa itakuwa faida kwa Mbape kuweza kupata nafasi za kufunga mabao zaidi.

"Ninaweza kusema kwamba nilikuwa ninashangazwa na uwezo wa Harry hasa katika namna ya ufungaji wa mabao, lakini unaweza kumtazama pia Karim, fikiria sasa yupo na Mbappe na wanacheza timu moja unadhani nini kitatokea, ninadhani kwamba kuna jambo moja kubwa linakuja.

"Karim atamfanya Mbappe kuwa bora na hicho alifanya Madrid mbele ya Cristiano. Kama ilivyo kwa Harry na Son Heung-min ni watu ambao wanavutia kimbinu katika kutengeneza nafasi na kufunga," .



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic