INJINIA Hersi Said ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Usajili ndani ya Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi amesema kuwa ikiwa Yusuf Manji atakuwa ndani ya Yanga basi timu hiyo itafanya vizuri Afrika.
Ujio wa Yusuf Manji ambaye alikuwa Mwenyekiti wa zamani wa Yanga na mdhamini pia nchini umekuwa gumzo hasa kuelekea katika uwekezaji ambapo habari zinaeleza kuwa anaweza kurejea ndani ya kikosi cha Yanga.
Hersi amesema:"Ujio wa Manji ni baraka kwetu na tumekuwa tukiita wadau wengi kuja kutuunga mkono GSM kwenye kuendesha timu yetu. Gharama ni kubwa tunalipa kambi na vitu vingine.
"Manji ni mdau wa Yanga na anaipenda timu hii akija kwa namna moja ama nyingine anaweza kuifanya timu hii ikawa bora zaidi Afrika," .
Mara ya mwisho Yanga kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara ilikuwa ni msimu wa 2017 likiwa ni taji lao la 27.
Manji alitua Bongo wiki hii baada ya kuwa nje ya nchi kwa muda. Wakati akiwa ndani ya Yanga aliweza kufanya usajili wa nyota wengi wakubwa ambao waliweza kuipa mafanikio timu hiyo na timu iliweza kutwaa mataji ikiwa ni pamoja na kombe la ligi.
Anajisemea tuu lakini moyoni anajua wazi manji akitua hersi na gsm yake kwisha maneno, itabidi warudi kuuza magodoro. Na sijui huyo anayejiita injia ni injia wa vitu gani, labda utapeli
ReplyDeleteKwa sababu akili zako zipo makalioni hatushangai kusoma uharo wako.Ukitaka kujua ni injinia wa vitu gani tafuta wasifu wake
DeleteYaani bwege sana wewe. Hii si timu ya mijusi fc inayomilikiwa na mtu mmoja.
DeleteHahaha hapo ni kama umejitukana mwenyewe, we unamiliki nini wakati mwenyekiti mwenyewe hana sauti, timu ipo chini ya Msomalo koko
DeleteUto bila manji haiwezekani.... Waliopo wame prove failure
ReplyDelete