June 5, 2021


IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Al Ahly, Walter Bwalya yupo kwenye hesabu za mabosi wa Kariakoo, Simba ambao wanahitaji kuipata saini yake.

Nyota huyo ambaye alicheza ndani ya kikosi cha Nkana FC ya Zambia kisha akaibukia Klabu ya El Gouna alikuwa kwenye rada za Simba kwa muda mrefu ila dau lilimkimbiza nyota huyo na kuibukia Al Ahly.

Kutokana na ushindani wa namba nyota huyo ameshindwa kufurukuta chini ya Kocha Mkuu, Pitso Mane jambo ambalo linafanya wafikirie kumuuza.

Wakala wa mshambuliaji huyo, Paricha Chikoye amesema kuwa ni kweli mchezaji huyo mabosi wake wanataka kumuuza.

"Ni kweli Al Ahly wanataka kumuuza mteja wangu kutokana na kuona kwamba haendani na mfumo ya timu yao.

"Imekuwa tetesi kwamba anahitajika na Simba ila hakuna mpango unaondelea kwa sasa kwa sababu hata mchezaji mwenyewe bado hajawa na mpango wa kuja huko," .

1 COMMENTS:

  1. Sasa hapo aliyewaambia Simba wanamtaka ni nani?? Maana nmeandika na hapohapo mnakanusha.... Msitufanye wajinga acheni mambo yenu ya kizushi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic