BADO kuna jambo la kufanya kwenye kikosi cha Yanga hasa katika suala la nidhamu ambayo inaonekana kuna mahali hapapo sawa.
Imekuwa kawaida kwa hivi karibuni kuwaona wachezaji wa Yanga wakizinguana wenyewe kwa wenyewe na muda mwingine na mashabiki wao jambo ambalo halina afya kwa maendeleo ya soka.
Ipo wazi kwamba kwa sasa kuna wachezaji wawili ambao wamewekwa kando na Yanga kutokana na ishu ya utovu wa nidhamu hivyo ni muhimu kuangalia wapi wanakwama.
Wakati wanajiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United wapo wachezaji ambao wamewekwa kando kutokana na ishu ya nidhamu.
Zipo timu nyingine ambazo zinafanya mambo hayo ila inakuwa ni nje ya uwanja na haionekani hadharani kama inavyotokea kwa Yanga.
Ikumbuke ishu ya Saido Ntibanzokiza namna alivyozinguana na wachezaji wenzake pamoja na kocha wa zama zile Juma Mwambusi ikiwa ni suala la kucheza na kufunga bao jambo ambalo alikasirika sababu ya kuanzia benchi.
Bado alibebwa na kuzungumza kwamba ilikuwa ni sehemu ya mchezo basi ikiwa kutakuwa na mwendelezo huu kuna mahali hapapo sawa.
Lamine Moro nyota wa Yanga ambaye ni nahodha pia amewekwa kando kwa muda kutokana na kile ambacho kimeelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
Nyota huyo amekuwa kwenye mvutano mkubwa na mabosi wake ambapo mara ya mwisho aliondolewa kwenye kambi ya timu hiyo ilipokuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC.
Baada ya hapo hajaonekana kwenye kikosi cha Yanga na hakuwa kwenye msafara wa kikosi kilichokwea pipa kuibukia Tabora kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United.
Mbali na Lamine pia kipa wao namba moja, Metacha Mnata naye pia hatakuwa sehemu ya kikosi kutokana na tatizo la utovu wa nidhamu.
Mnata alisimamishwa hivi karibuni baada ya kuonyesha ishara isiyo na tafsri nzuri kwa mashabiki jambo ambalo limefanya nyota huyo asimamishwe.
Basi kwa kuwa Yanga ni timu kongwe inapaswa kuwa mfano kwa Mwadui FC, Gwambina, Njombe Mji pamoja na Kagera Sugar ambao hawajawa na matukio ya namna hii.
Itazame namna Polisi Tanzania inavyoshughulikia masuala ya nidhamu, ilisimamisha wachezaji wake wote ambao walikuwa na mwendo mbovu na wale ambao waliweza kujirekebisha walirudi kikosini.
Iwe hivyo kwa kila timu mafanikio yanabebwa na nidhamu.
Tatizo hawa wamedhulumiwa na wakidai chao wanajikuta wanaangukia kwenye utovu wa nidhamu
ReplyDeletemkude muhimbili nae kadhulimiwa au mhaho?
DeleteHao msingi wao ni matatizo yasiyokwisha na bila ya matatizo hawaoni raha hata kidogo
ReplyDeleteSaleh Jembe hivi mbona hauachi upuuzi wako wa kutumiwa na vibaraka vya Simba Sc na kulipwa na Mo ili uichafue Yanga kwa taarifa yako Yanga ni kubwa sana….. Yanga ndio baba wa soka la Tanzania ndiyo klabu ya kwanza kuzaliwa propaganda zake na uzushi wako hautafanikiwa. Kaandikeni ya akina Jonas Mkude kupelekwa Muhimbili achana na habari za wachezaji wa Yanga
ReplyDeleteHuenda ikawa hao kama ilivo kwa Mnata, akicheza bila ya malipo na baadae ikaishia kuzomewa na kutengwa
ReplyDeleteAlways Harmony kwa Yanga Ina mkwaza huyu brother so niulize Saido Ana kosa gani Kaka so alicheza juzi au tusemeje
ReplyDeleteWaandishi uchwara..!
ReplyDeleteHivi unajuwa umepoteza mvuto saleh juzi morisson kazingua hukuona tumekuchoka acha ushamba unaandika vitu vya uongo juzi uumesema mazembe ya izidi yanga leo ktk wachezaji 7 nae yupo mbona unahalibikia ukubwani kama bamia
ReplyDelete