DILI la usajili wa mshambuliaji wa Horoya AC ya Guinea, Heritier Makambo limekamilika kwa asilimia 70 na kilichobakia ni kwa mabosi wa GSM kuifuata timu yake hiyo kwa ajili ya kufikia muafaka.
Makambo ni kati ya wachezaji waliokuwa kwenye mipango ya kusajiliwa na Yanga katika usajili wa msimu ujao katika kuisuka safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Hii siyo mara ya kwanza kwa Yanga kupanga kumrejesha mshambuliaji huyo kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo aliyeondoka msimu wa 2018/2019.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, mshambuliaji huyo amekubali kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja alioubakisha kwa sharti la mabosi hao kumfuata kwa ajili ya mazungumzo yatakayofikia muafaka mzuri.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa ni ngumu kwa Makambo kuandika barua ya kuondoka kwa uongozi wa Horoya kabla ya uongozi wa Yanga kumfuata kwa ajili ya mazungumzo.
Aliongeza kuwa mchezaji mwenyewe ameonyesha nia ya kutaka kuondoka Horoya baada ya kuona hapati nafasi ya kucheza katika kikosi hicho.
“Yapo mengi yanayoendelea kati ya Horoya na Makambo ambaye yeye amekubali kuandika barua kwa uongozi wa timu yake ya kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja ili aje ajiunge na Yanga katika msimu ujao.
“Makambo akiwa huko kocha wake anamtumia kucheza winga ambayo haitaki, yeye anataka kucheza namba 9 au 10 ambazo amekuwa akizicheza.
“Hivyo kitendo cha kukataa nafasi hiyo kimemfanya kocha wa Horoya kumuweka benchi, kwake kimeonekana kumkasirisha na kufikia hatua ya kutaka kuomba kuondoka hapa lakini anashindwa kutokana na kutopata timu, hivyo kama Yanga wakimfuata haraka ataandika barua ya kusitisha mkataba ili aondoke,” alisema mtoa taarifa huyo.
Championi Jumatano, lilimtafuta Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Wapo wachezaji wengi walio katika mipango yetu ambao ni siri, tumepanga kuwatambulisha mara baada ya kumaliza taratibu zote za usajili.
”Makambo mwenyewe hivi karibuni aliandika ujumbe kwenye mtandao wa jamii uliosomeka hivi: “Nimewamisi Yanga, nimewamisi mashabiki wa Yanga.”
Ingekuwa Makambo mchezaji mzuri alienunuliwa kwa mkwanja mkubwa, kocha asingemuweka benchi na kukataa kocha kumuweka namba 9 bila ya shaka kaona hauwezi, haya endeleeni lakini asije kuzomewa
ReplyDeleteDouble kick,Pombe za kupima,Mirungi,Jani la Arusha nk na mengine mengi yanayo yanayowatoa ufahamu yasiwe sehemu ya kupinga mpaka ukahukumu hizi Ni tetesi na Mwandishi hii Ni sehemu ya kazi yake lkn najua ingefavour upande wako ungesupport lkn zingatia Football is always about fareplay
ReplyDelete